Home Kitaifa FEDHA ZA TOZO NDIO ZINAZOTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO-STEVE NYERERE

FEDHA ZA TOZO NDIO ZINAZOTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO-STEVE NYERERE

Na Magrethy Katengu

Msanii wa Bongo Movie Steve Mengele” Steve Nyerere” amewasihi Watanzania kuendelea kuchangia kodi kupitia tozo za miamala ya benki na simu kwa madai kuwa tozo hizo zinasaidia kuleta Maendeleo Kwa Taifa.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na wanahabari ambapo amesema kwamba jambo la tozo lipo duniani kote na kwamba ni Jambo ambalo la tija kwa Taifa kutokana na kutatua changamoto mbalimbali za Maendeleo Kwa wananchi.

Hata hivyo amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuwafikisha watanzania kufikia hatua ya Maendeleo ya kujivunia wenyewe kufanya miradi mikubwa kwa fedha zao na kuondokana na kutegemea fedha za hisani kutoka mataifa ya nje ikiwemo Ulaya,Asia na Marekani.

” Tozo hizi zipo duniani kote,tusiweendekeze maneno ya siasa pamoja na vikundi vinavyojiita wanaharakati ifike mahali fedha zetu watanzania wote tujivunie na tozo zikijenga miradi ukipita imeandikwa ni jasho la wananchi hivyo ,kama tozo hii ina ( tatizo) kidogo inaweza kusawazishwa tu kwa kupunguza na siyo kuiondoa kabisa” amesema Steve.

Amesisistiza kuwa tozo hizo zinasaidia kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo kujenga Barabara ,Madaraja,Reli ya Kisasa,Hospitali ,na miradi mingine ya maendeleo,hivyo watanzania wanapaswa kushikamana na serikali katika kutekeleza Ujenzi wa miradi hiyo kupitia tozo wanazokatwa .

Sanjari na hayo amesema kuwa endapo Watanzania watatekeleza tozo hizo watakuwa wameonyesha uzalendo wa hali ya juu kwani hata nchi zingine zilizoendelea akitolea mfano China, Singapore,na Malasia zinategemea kodi kutokana na tozo.

“Kuna wengine tumewaona wanaenda Mahakamani kupinga tozo hizi,pia kuna wasanii wanakurupuka kutunga nyimbo za tozo nimezungumza na BASATA isiruhusu nyimbo hizo za upotoshaji,kwani uhuru tukiuruhusu sana utatugawanya” amesema.

Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba Viongozi wa Dini,Wanasiasa,na Waandishi wa habari kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa tozo zinazotozwa kwenye miamala ya kibenki na simu ili kuondoa sintofahamu Kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!