Na Adery Masta.
Benki ya Equity inajivunia kuendelea kuwa na mikakati thabiti kwa ajili ya wakulima Nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali kama vile pembejeo , Trekta na Mitaji ambapo tangu mwaka uanze benki iyo imeweza kutoa mikopo ya Shilingi Bilioni 46 ikiwa ni katika mazao ya mahindi , pamba , Alzeti n.k
Hayo yamebainishwa Leo Julai , 02 , 2024 na Meneja Mkuu wa Biashara – Equity Bank Bi. Leah Ayoub wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Banda lao jipya kabisa katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa Sabasaba , lililoko Maonesho Avenue Viwanjani humo .
Aidha Bi. Leah amesema Equity Bank imejipanga kisawasawa kuwahudumia wateja watakao tembelea banda lao katika maonesho hayo
” Tunawakaribisha sana wateja wetu , msimu huu wa sabasaba tuna ofa mbalimbali kwa ajili ya wateja wetu wadogo na wakubwa Huduma kama kutoa na kuweka fedha , Mikopo midogo na mikubwa , Huduma ya Benki Kidigitali kupitia HAPO HAPO AKAUNTI rahisi kabisa kwa kupiga *150*07# , Simu yako Benki yako popote ulipo utapata huduma za EQUITY Benki ikiwemo kufungua akaunti “ amesema
Aidha amewasisitiza wakulima kuchangamkia fursa hii ya Mikopo na huduma nyingine kibao za benki iyo hasa msimu huu wa sabasaba.