Home Kitaifa DKT. KIJAJI AIAGIZA KAMPUNI YA KUUNGANISHA MAGARI KUONGEZA NGUVU NA KASI

DKT. KIJAJI AIAGIZA KAMPUNI YA KUUNGANISHA MAGARI KUONGEZA NGUVU NA KASI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ameiagiza Kampuni ya GF Trurcks & Equipment kuongeza nguvu na kasi ya kuunganisha magari makubwa na vifaa vya ujenzi na madini ili kuhudumia Afrika na upitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika pamoja na Dunia nzima kwa ujumla.

Waziri Kijaji ameyasema hayo Julai 04, 2022 katika Hafla ya kusherekea miaka 15 ya Kibiashara ya Kampuni ya GF Trucks wakati wa Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere barabara ya Kilwa – Dar es Salaam yaliyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2022.

Waziri Kijaji pia ameishauri Kampuni hiyo pamoja na wafanyabiashara wote kuwa waaminifu na waadilifu ili kujenga imani na wateja na kuweza kuhudumia Afrika na Dunia kwa ujumla.

Waziri pia amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini pamoja na kuondoa vikwazo mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint for Regulatory Reforms) ambapo baadhi ya changamoto zimetatuliwa kuisha kabisa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Imran Kamali amesema Kampuni hiyo iliyofanikiwa kuunganishwa magari 600 na kutoa ajira kwa wafanyakazi 300 inaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuongeza uzalishaji ambao utaingeza ajira na pato la Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!