Home Kitaifa DIWANI PAZI AISHUKURU TAASISI YA ABDULLAH AID, YAWASAIDIA WENYE MAHITAJI MAALUM

DIWANI PAZI AISHUKURU TAASISI YA ABDULLAH AID, YAWASAIDIA WENYE MAHITAJI MAALUM

Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe. Busoro Pazi kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Buguruni ameishukuru Taasisi ya Abdullah Aid yenye makao yake Makuu Nchini Uingereza kwa kupitia Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Tawi la Tanzania Shekhe Arif Suriya kwa kukubali maombi yake ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum (Walemavu) kwa kuwapatia msaada wa baiske maalum 18.

Diwani huyo pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri kwa Taasisi za ndani na nje ya nchi kuweza kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kuinua ustawi wa nchi yetu kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!