08/ DEC 2023
Katibu wa NEC Idara ya Organaizeaheni CCM Taifa Issa Gavu amekuwa mgeni Rasmi katika kikao cha Baraza la wazee Mkoa wa Kilimanjao kilichohudhuriwa na wajumbe wa baraza kutoka wilaya zote za mkoa wa kilimanjaro wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Patrick Boysafi.
Gavu amepata muda wakuzungumza na kushauriana na wazee wa Mkoa wa kilimanjaro na kupokea Maoni, Ushauri na Busara za namna ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake.
Pamoja na Mambo mengine Gavu aliwasihi wazee waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kukishauri katika ngazi zote ili kuleta tija na Ufanisi mzuri katika kuwaongoza wananchi waliotupa ridhaa ya kuiongoza Serikali.
Aidha, Gavu aliendelea kukemea vikali viongozi wenye tabia ya kutafuta nafasi ya uongozi kwa madhumuni yakujinufaisha yeye binafsi ama familia yake.
“Kiongozi mwenye tabia kama hizo chama Cha mapinduzi hakitakuwa tayari kumpitisha mtu wa namna hiyo” Amesema Issa Gavu
“Tunaitaji kiongozi ambae akisimama mbele za watu, jamii inakubali inasema naam huyu anastahili na anasifa za kuwa kiongozi wetu” Amesema Issa Gavu
“Tunaitaji kiongozi ambae anajua dhamana aliyopewa, anajua madhumuni aliyopewa, anajua changamoto alizozibeba na anajua dhima na Jukumu alilokabidhiwa na Chama Chetu kwa jamii anayoiongoza” Amesema Issa Gavu
“Kiongozi ambae hayupo tayari kuhangaika na majambo ya watu anaowaongoza kiongozi huyo atusamehee, tunaitaji kiongozi awe mfano mbele ya Jamii anayoiongoza” Amesema Gavu.
“Hatutoweza kupata kiongozi mwenye sifa hizo zinazoakisi sifa za Cha Cha Mapinduzi nje na Chama Cha Mapinduzi, Sote ni mashahidi na tumeridhika na mwenendo wa Mwenyekiti wa CCM na Rais Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyojitoa kwa sisi anaotuongoza”
“Kigezo na Mfano wetu, tunaitaji kiongozi ambae yupo tayari kuhangaika na mambo ya watu anaowaongoza, huyo ndiyo kiongozi tunaemuhitaji” Amesisitiza Gavu