Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo. Jenerali Mabeyo alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga Mhe. Rais Samia wakati akimaliza kipindi cha Utumishi wake katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.