
Kinshasa, 17 Agosti 2026: Airtel Africa imeandika historia baada ya kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano barani Afrika kuzindua kibiashara intaneti ya satelaiti kwa simu nchini Jamhuriya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikifungua ukurasa mpya katika upatikanaji wa mawasilianokatika maeneo yasiyofikiwa na minara ya kawaida ya simu.
Huduma hiyo, inayotolewa kupitia ushirikiano kati ya Airtel Africa na Starlink, inawezeshawateja wenye simu janja zinazooana kupata huduma za mawasiliano katika maeneo ambayohayafikiwi na miundombinu ya kawaida ya mawasiliano ya simu.
Starlink ina zaidi ya satelaiti 650 zinazosaidia huduma za mawasiliano ya moja kwa moja kati yasatelaiti na simu (satellite-to-mobile). Kwa sasa, huduma hiyo inalenga matumizi ya programuzinazotumia kiwango kidogo cha data, ikiwemo ujumbe wa WhatsApp, pamoja na SMS, bilakuhitaji wateja kuwa na vifaa maalumu au kifaa cha ziada.
Uzinduzi huo unafuatia makubaliano ya kimkakati yaliyotangazwa na Airtel Africa na Starlinkmwezi Desemba 2025, pamoja na majaribio ya huduma za data na ujumbe nchini Kenya mweziMachi 2026.
DRC imekuwa soko la kwanza la Airtel Africa na nchi ya kwanza barani Afrika ambako hudumaya intaneti ya satelaiti kwa simu (Starlink Mobile) imefikia hatua ya kutolewa kibiashara.
Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Sunil Taldar, alisema hatua hiyo ni muhimu katika kupanua upatikanaji wa mawasiliano barani Afrika.
“Uzinduzi wa kwanza kabisa wa kibiashara wa Starlink Mobile barani Afrika ni hatua muhimukwa Airtel Africa kupitia ushirikiano wetu na SpaceX. Kwa kuunganisha mtandao wa Airtel waardhini na teknolojia ya satelaiti ya Starlink, tunapanua upatikanaji wa mawasiliano muhimuzaidi ya mipaka ya miundombinu ya kawaida ya simu. DRC inaongoza katika hatua hii muhimuya maendeleo, na uzoefu unaopatikana hapa utasaidia katika kupanua huduma hii hatua kwahatua katika masoko yetu, kwa kuzingatia idhini za mamlaka za udhibiti za kila nchi.
“Ninapenda kutambua kwa namna ya pekee na kutoa shukrani zangu kwa Serikali ya Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo kwa msaada wake muhimu katika kufanikisha hatua hii, hususan kupitiaMheshimiwa Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia Mpya ya Habari na Mawasiliano, Raiswa Mamlaka ya Udhibiti pamoja na timu zao.”
Taldar alisema uzoefu unaopatikana DRC utasaidia Airtel Africa katika kupanua huduma hiyokatika masoko mengine ya kampuni, kwa kuzingatia idhini na matakwa ya mamlaka za udhibitikatika kila nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel DRC, Thierry Diasnoma, alisema hudumahiyo ya satelaiti itaongeza fursa za mawasiliano katika nchi yenye eneo kubwa kijiografia, ambako baadhi ya wananchi wanaishi, kufanya kazi au kusafiri mbali na miundombinu yakawaida ya mawasiliano.
“Huduma hii ya intaneti ya satelaiti kwa simu inatoa safu ya ziada ya mawasiliano, ikisaidiawateja kuendelea kupatikana, kupata taarifa na kuwasiliana katika maeneo ambayo mtandao waminara haupatikani,” alisema Diasnoma.
Huduma ya intaneti ya satelaiti kwa simu inalenga pia kuwasaidia wasafirishaji na kampuni za usafirishaji na usambazaji, mashirika ya kibinadamu, wahudumu wa afya, wakulima, kampuni za uchimbaji madini na jamii zinazoishi katika maeneo ambayo hayajafikiwa kikamilifu namitandao ya ardhini.
Aidha, teknolojia ya intaneti ya satelaiti kwa simu inaweza kuwa nyenzo muhimu katikamawasiliano ya dharura wakati wa majanga ya asili au pale ambapo mtandao wa kawaidaunakatika kwa muda.
Kwa sasa, wateja wanaotaka kutumia huduma hiyo wanapaswa kuwa na simu janja ya Android yenye LTE inayooana na mfumo wa Starlink Mobile, pamoja na kifurushi cha data cha Airtel DRC kinachokidhi vigezo au huduma ya data roaming iliyowashwa.
Airtel imesema simu na vifaa vya kampuni ya Apple, vitawezeshwa kutumia huduma ya intanetiya satelaiti kwa simu katika siku zijazo.
Wateja wanaokidhi vigezo wanaweza kujisajili kupitia MyAirtel App na kupata huduma yamajaribio bila malipo kwa siku 30 za kwanza.
Wateja wanaosafiri kwenda DRC na kujiunga na Airtel DRC wanaweza pia kujisajili kwahuduma hiyo ya majaribio baada ya kuamilisha huduma inayokidhi vigezo na kupakua MyAirtelApp.
Baada ya kipindi cha majaribio, huduma itaendelea kupatikana kupitia vifurushi vya data vyaAirtel vinavyokidhi masharti.
Airtel Africa na Starlink zimesema zinaendelea kuboresha huduma hiyo, huku uwezo wa ziadaukitarajiwa kuongezwa kadri teknolojia inavyoendelea kukua na idhini za udhibitizinavyopatikana.
Uzinduzi huo unaiweka Airtel Africa katika nafasi ya kampuni ya kwanza ya mawasiliano baraniAfrika kuanza kutoa intaneti ya satelaiti kwa simu kibiashara, huku ikiendelea kutumiateknolojia mpya kupanua wigo wa mawasiliano na kuongeza ujumuishwaji wa kidijitali baraniAfrika.









