Home Kitaifa MBUNGE AGNES AOMBA MIRADI YA MAJI VIJIJI VYA SERENGETI

MBUNGE AGNES AOMBA MIRADI YA MAJI VIJIJI VYA SERENGETI

Na Shomari Binda

MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Mara,Agnes Marwa,ameiomba serikali kupeleka miradi ya maji kwenye vijiji vya Serengeti ili kumtua mama ndoo kichwani.

Maombi ya mbunge huyo yametolewa leo bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye Wizara ya Maji.

Akiuliza swali la nyongeza mbunge Agnes alitaka kujua ni lini serikali itawafikishia maji wananchi wa vijiji vya Serengeti ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji na maeneo mengine ya mkoa wa Mara.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi, amesema serikali inaendelea kufikisha huduma ya maji safi na salama maeneo mbalimbali na vijiji vya Serengeti vitafikiwa.

Naibu Waziri huyo wa maji amemshukuru mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwasemea wananchi hususani katika masuala ya maji.

” Nimshukuru sana mheshimiwa mbunge kwa swali lake nimuhakikishie kuwa wananchi wa Serengeti na maeneo mengine ya mkoa wa Mara yatafikiwa na huduma ya maji”,amesema Mahundi.

Bunge linaendelea jijini Dodoma kwa wabunge kuchangia kwenye Wizara ya Maji kwa kuwasilisha michango mbalimbali ya maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!