Home Kitaifa WAZIRI KIKWETE AMJULIA HALI MAMA KARUME, APELEKA SALAMU ZA RAIS SAMIA

WAZIRI KIKWETE AMJULIA HALI MAMA KARUME, APELEKA SALAMU ZA RAIS SAMIA

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani  Kikwete, akizungumza  na Mama Fatuma Karume mara baada ya   kumtembelea  nyumbani kwake Unguja, Zanzibar kwa lengo la kumjulia hali

Na Lusungu Helela, Unguja

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amemtembelea Mama Fatuma Karume nyumbani kwake Unguja, Zanzibar na kumfikishia salamu za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mhe. Kikwete amefika nyumbani kwa Mama Karume kwa lengo la kumsalimia, kumjulia hali na kusikiliza changamoto alizonazo na kuzitafutia ufumbuzi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kama Waziri mwenye dhamana ya kuwatunza viongozi Wakuu Wastaafu wa kitaifa na wenza wao.

“Rais Mheshimiwa Samia amenielekeza nikufikishie salaam zake na amesema yuko pamoja nawe. Ndiyo maana amenituma kufika hapa nyumbani na kukujulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi,” amesema

Aidha, Waziri Kikwete ameahidi kuwaelekeza watendaji katika ofisi yake kushughulikia changamoto zinazojitokeza ili familia za viongozi na wenza hao ziendelee kuishi kwa amani na usalama.

Amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

Kwa upande wake, Mama Karume amemshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote bila kuchoka.

Amemuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia Watanzania.

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Ridhiwani  Kikwete, akisalimiana na Mama Fatuma Karume mara baada ya  kumtembelea  nyumbani kwake Unguja, Zanzibar kwa lengo la kumjulia hali

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani  Kikwete, akizungumza  na Mama Fatuma Karume mara baada ya   kumtembelea  nyumbani kwake Unguja, Zanzibar kwa lengo la kumjulia hali

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani  Kikwete, akimkabidhi zawadi ya ua  Mama Fatuma Karume mara baada ya  kumtembelea  nyumbani kwake Unguja, Zanzibar kwa lengo la kujulia hali 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Nyasinde Mkono akiwa kwenye picha ya pamoja  na Mama Fatuma Karume mara baada ya kumtembelea  nyumbani kwake Unguja, Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!