Home Kitaifa TAASISI 300 ZASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU, SAYANSI TANGA

TAASISI 300 ZASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU, SAYANSI TANGA

Na Boniface Gideon, TANGA

Taasisi 300 zimeshiriki maonyesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amewaambia waandishi wa habari leo Agosti 17 kuwa maonyesho hayo yalianza rasmi Agosti 15 na yatafungwa Agosti 24, ambapo yanatarajiwa kufunguliwa Agosti 18 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Balozi Batilda alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya pili mkoani Tanga, ambapo mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2024 katika viwanja vya Popatlal jijini Tanga.

Batilda alisema ujio wa maonyesho hayo unatoa fursa kwa wakazi wa Jiji la Tanga kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo,

Kwetu sisi wakazi wa Jiji la Tanga ni fursa kubwa kiuchumi. Wafanyabiashara mbalimbali wa Mkoa wa Tanga ni vyema kila mmoja akachangamkia fursa za maonyesho haya, mama lishe, wamiliki wa hoteli pamoja na boda boda, pamoja na wadau mbalimbali waitumie fursa hiyo,” aliongeza Batilda.

Balozi Batilda aliwataka wakazi wa Jiji la Tanga pamoja na mikoa ya jirani kufika kujionea ubunifu wa teknolojia mbalimbali uliofanywa na wataalamu wa ndani,

Nawaomba wakazi wa Mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani, mje kujionea ubunifu wa teknolojia mbalimbali uliofanywa na wataalamu wa ndani ya nchi yetu, lakini pia kama kuna mtu yeyote mwenye ubunifu wa kitu chochote ni vizuri ukafika kuonyesha ulichonacho, utakutana na wataalamu na taasisi mbalimbali na utasaidiwa, na utaweza kupata fursa ya kuonyesha ulichonacho,” alisema Balozi Batilda.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!