Home Kitaifa RC BATILDA AUNDA TUME KUCHUNGUZA BOMOA BOA MSAKANGOTO

RC BATILDA AUNDA TUME KUCHUNGUZA BOMOA BOA MSAKANGOTO

Na Boniface Gideon, TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt. Batilda Burian,ameunda tume maalum yenye wajumbe 6 kwaajili ya kuchunguza sakata la bomoa boa wa makazi ya waliokuwa wafanyakazi wa kampuni moja ya Mkonge katika kijiji cha Msakangoto wilayani Muheza.

Ubomoji wa nyumba 67 ulifanyika hivi karibuni na moja ya kampuni ya udalali mkoani Tanga mara baada ya kampuni ya Mkonge kushinda kesi Mahakamani.

Akitangaza kuundwa kwa tume hiyo kwa Waandishi wa Habari, Balozi Batilda amesema,tume hiyo itakuwa na kazi yakufanya tathmini yakina bila upendeleo ama kumuonea mtu juu ya nani aliyetoa vibali vya kuvunja makazi ya Wananchi bila utaratibu nakwamba itafanya kazi kwa siku 5,

” Tume hii itakwenda kusadia kuchunguza kwakina kwanini wavunjaji walichukua maamuzi yakuvunja makazi ya Wananchi bila utaratibu wa vibali na kiukweli kwenye uchunguzi huu usipendelee wala kumuonea mtu”Alibainisha Dkt.Batilda

Dkt. Batilda alisema siku ya ubomoji wa nyumba 67 ulifanyika bila kuwepo kwa taarifa kuanzia Serikali ya Mtaa hadi Mkoa,

“Siku ya ubomoji wa nyumba 67 ulifanyika bila kuwepo kwa taarifa kuanzia Serikali ya Mtaa hadi Mkoa, lakini pia siku hiyo Viongozi wa Wilaya na Mkoa hawakuwepo ,hivyo dalali alitumia fursa hiyo kwaajili ya kuhalalisha kazi yake ili apate malipo, lakini haya yote tume hii italeta majibu ambayo yatatusaidia kupata majibu na suluhisho la kudumu”Alisisitiza Dkt.Batilda

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!