Na Shomari Binda-Muwasa
WATUMISHI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi 8 wa Mazingira Musoma (MUWASA) wamepewa mafunzo ya kujengewa uwezo ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa wateja.
Akizungumza na watumishi hao kabla ya kuanza kwa mafunzo yaliyoendeshwa na kampuni ya Cledit & Debit Master Company Limited (CDM) mkurugenzi mtendaji wa Muwasa Nicas Mugisha amesema mafunzo ni sehemu ya ufanisi.
Amesema ili mtumishi aweze kufanya kazi take vizuri ni vyema kupewa.mafunzo ya mara kwa mara ili kumjengea uwezo zaidi.
Nicas amesema mafunzo hayo ambayo yata yanazingatia pia ukusanyaji mapato yataisaidia pia idara ya ukusanyaji madeni wa mamlaka ili kufnanya kazi vizuri.
Mkurugenzi huyo amesema kila mmoja akizingatia mafunzo hayo yaliyotolewa yatasaidia mamlaka katika utendaji.
“Mafunzo kwa watumishi yataleta chachu ya utoaji wa huduma bora kwa wateja wa mamlaka ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na madeni ya muda mrefu yaliyopo kwa wateja walisitishiwa huduma ya maji”
“Uongozi wa Muwasa umeandaa mafunzo haya tukiamini utaleta manufaa makubwa kwenye mamlaka na kupata mafanikio” ,amesema Nicas.
Kwa upande wa watumishi walioshiriki mafunzo hayo wameushukuru uongozi kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia.
Aidha watumishi hao wamemshukuru mkurugenzi wa Muwasa kwa kuwa karibu na watumishi na kuwasikiliza pale wanapomfikia.









