Home Kitaifa WATENDAJI WA SENSA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

WATENDAJI WA SENSA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es salam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza jambo kabla ya kikao na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Prof.Riziki Shemdoe kabla ya kikao.

Na mwandishi wetu

Watendaji wa Sensa wapewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi  zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 August 2022, wito huo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene.

“baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuna kazi kubwa ya Mchakato lazima tuwe tayari kusimama pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili zoezi liweze kukamilika

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es saalam.

Waziri Simbachawene ameipongeza kamati ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kufanikisha maamuzi ya kamati kuu ya Taifa ya Sensa.

Vilevile napongeza Wizara zote, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi kwa ushirikiano mkubwa  walioonesha wakati wote wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa amesema kwa wakuu wa kaya ambao hawatakuwa nyumbani wameandaa fomu maalumu ambayo itakuwa na maswali 11 ambayo itasambazwa kwa wakuu wote wa kaya kupitia kwa makarani wao wa sensa.

Wakuu wa kaya waandike taarifa za watu ambao watakuwa wamelala usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kumrahisishia karani kujaza taarifa kwenye kishikwambi atakapofika kuchukua taarifa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!