Home Kitaifa WATANZANIA NAO WASHIRIKISHWE KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI

WATANZANIA NAO WASHIRIKISHWE KWENYE MIRADI YA KIMKAKATI

Na Magrethy Katengu

Watanzania wanakabiliwa na changamoto ikiwemo ya Ukosefu wa ujuzi, kukosekana kwa sera ya kitaifa, ushirikikishwaji hafifu wa jamii, miundombinu duni, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa malighafi, uwezo mdogo wa uzalishaji bidhaa bora ndiyo na kupelekea kutoshirikishwa katika miradi ya kimkakati ya serikali..

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdah wakati akifungua kikao cha wadau cha kujadili taarifa ya tathimini ya Ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Miradi ya kimkakati ambapo amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali lakini bado changamoto zipo hivyo ni vywema hatua za makusudi zikachukuliwa ili kuwakwamua watanzania kiuchumi kwa kuwa na miongozo inayoongoza ushirikishwaji katika Miradi ya kimkakati.

Sote tunatambua kuwa hakuna nchi yeyote iliyopiga hatua kubwa kimaendeleo na kufanikiwa bila kuweka dhamira na jitihada za makusudi za kuhakikisha kunakuwa na Mazingira wezeshi kwa wananchi kushiriki ipasavyo kwenye uwekezaji miradi ya kimkakati..

Pia Dkt Abdalah amesema serikali imechukua hatua za makusudi zinazolenga kukuza ushirikishwaji katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaonufaisha watanzania ikiwemo makampuni yanayoanzishwa kwa sekta binafsi kuingia ubia nao ili kupitia hiyo mapato yanayotoka yanufaishe watanzania kwa kuwasaidia kupata huduma muhimu ikiwemo maji, Afya, Elimu na miundombinu .

Naye Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng’ Issa amesema japo Watanzania wanashiriki Miradi ya kimkakati lakini si kwa asilima mia Moja lakini utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa tangu mwaka 2015 Watanzania wamekuwa ushiriki wao katika miradi ya kimkakati idadi Yao ikiongezeka na kusaidia kupata fursa za ajira mbalimbali kwa Vijana ikiwemo udereva, ununuzi bidhaa, usafirishaji, uhandisi,

Kwa Upande wake Mkurugenzi Miradi Shirika la Maendeleo Umoja wa Mataifa (UNDP) Amoni Manyama amesema sekta binafsi zilizopo hapa nchini ni zina uwezo wa kuingia ubia katika miradi ya kimkakati na kuweza kusaidia watanzania wenzao hususani Vijana kupata fursa za ajira

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!