Home Kitaifa WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI PROF.MUHONGO UJENZI SHULE SHIKIZI KITONGOJI CHA NYASAENGE

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI PROF.MUHONGO UJENZI SHULE SHIKIZI KITONGOJI CHA NYASAENGE

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kitongoji cha Nyasaenge Kijiji cha Kataryo Kata ya Tegeruka,wameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule.

Licha ya kuishukuru serikali lakini pia wamemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Prof.Sospeter Muhongo, kwa kuchangia mifuko ya saruji na vifaa vya ujenzi kuchangia elimu.

Shukrani hizo wamezitoa wakati Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma vijijini ya CCM na mbunge Muhongo walipotembelea shule shikizi ya Nyasaenge.

Wananchi hao wamesema shule hiyo imesaidia watoto wao kusoma jirani tofauti na mwanzo walipokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Wamesema kupitia shule hiyo iliyopo kwenye Kitongoji hicho watoto wamekuwa wakihudhuria darasani na kupata elimu pasipo changamoto za kutembea umbali mrefu

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Musa Magoti,amesema serikali na mbunge Muhongo wamechangia nguvu za wananchi kuwepo kwa shule hiyo.

Kitongoji cha Nyasaenge ni moja ya vitongoji sita (6) vya Kijiji cha Kataryo.vilivyopo Kata ya Tegeruka katika jimbo la Musoma Vijijini.

Mwaka 2017 wananchi wakazi wa Kitongoji cha Nyasaenge waliamua kushirikiana na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kujenga shule shikizi ili kutatua tatizo la watoto wao kutembea mwendo wa takribani kilomita 6 hadi8 kwenda na kurudi kutoka masomoni kwenye shule ya msingi Kataryo.

Ujenzi wa awali wa gharama ya shilingi milioni 49.01 ulikuwa wa vyumba vya madarasa viwili (2), ofisi ya walimu moja (1), choo chenye matundu manne (4)ikiwa ni michango na nguvukazi ilitolewa na wananchi wa Kitongoji cha Nyasaenge na mbunge Muhongo alichangia saruji mifuko 100 na mabati 108.

Baadae serikali mwaka 2021 ilitoa milioni 46,600,000
mwaka 2023 ilitoa fedha za Boost shilingi milioni 81,300,000 na baadae kutoa milioni 50,000,000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu.

Kwa sasa shule shikizi ya Nyasaenge imetimiza vigezo vyote vya kuandikishwa kuwa shule ya msingi kamili- ombi ambalo lipo kwenye halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!