Home Kitaifa WANAFUNZI BARA, VISIWANI WASHIRIKI KONGAMANO LA SAYANSI TANGA STEM PARK

WANAFUNZI BARA, VISIWANI WASHIRIKI KONGAMANO LA SAYANSI TANGA STEM PARK

Na Boniface Gideon, TANGA

ZAIDI ya wanafunzi 60 wa shule Sekondari kutoka katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania wameshiriki kikamilifu Kongamano la saba la sayansi na Teknolojia lililoandaliwa na Kituo Cha Sayansi Tanga STEM PARK chini ya usimamizi wa Project Inspire wakifuzu na kuonyesha umahiri katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya Nchi kupitia sayansi, Uhandisi na Hisabati.

Akifunga kongamano hilo la saba mwishoni mwa wiki Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana ameipongeza shirika la botna ambao ni wafadhili wa miradi mbalimbali inayotekelezwa jijini humo ikiwemo kituo cha Stem Park pamoja na walimu wanaowafundisha vijana na wanafunzi akiwataka mbali na Elimu kuwafundisha pia maadili mema.

Tunatambua mchango mkubwa sana wa botna foundation Ni Mengi Sana wametusaidia katika nyaja ya kielimu kijamii na hata afya pia wametoa Madawati ya shule za msingi Milion 286.3 , Mambo ya usalama barabarani wametoa million 442.5 , wamejengea uwezo kiuchumi vijana million434.9 hii miradi yote ni maendeleo makubwa ndani ya jiji la Tanga kwaajili ya wananchi” alisema Dkt. Liana

Akizungumza na wanafunzi hao amewataka kusimamia ndoto zao kujikita kimasomo zaidi kuhakikisha zinafanikiwa akiwataka kujiepusha na tamaa maswala ya ukatili ambayo yataweza kuharibu malengo yao waliyojiwekea huku akiipongeza kituo cha Stem Park kwa uwezeshaji huo kwa vijana.

Jilindeni vijana na jitunzeni msome kwa bidii ili mfikie lengo wazazi wenu wafurahi na mtapata baraka nyingi kwa wazazi , Mambo ya uzinzi , ukahaba ushoga , usagaji achaneni nayo zingatieni masomo yenu mfikie malengo yenu nawatakia kila la kheri” alisema Dkt. Liana

Mratibu wa makongamano hayo Dkt. Isaya Ipyana alisema kuwa wanafunzi hao ambao waliweka kambi kwa zaidi ya siku 5 katika kituo cha Sayansi Stem Park wamekuwa wakiwaelekeza namna gan ya kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi pindi wanapokuwa mashuleni na hata baada ya kumaliza elimu yao ambapo wataweza kutumia sayansi Teknolojia uhandisi na mahesabu ambayo walifundishwa kwa nadharia darasani na hivyo kufanya kwa vitendo hatua ambayo wakifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kongamano la mwaka huu tulikuwa tumelenga hasa kwenye changamoto ya mabadiliko ya tabianchi jinsi gani ambavyo watatumia sayansi uhandisi na mahesabu kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwahiyo kuanzia tarehe 26 mpaka 30 June wanafunzi kutoka Mikoa 10 ya Bara na Visiwani waliokuwa pamoja kukaa chini na kuutafuta njia mbadala ambazo wanaweza kuzitumia” alisema

“Wapo ambao waliwez kutengeneza ndege nyuki ( drones), wapo ambao waliweza kutengeneza mitambo kwaajili ya gesi, kwahiyo Nia kubwa Ni kuhakikisha Yale ambayo waliweza kujifunza darasani kwa nadharia wajifunze kwa vitendo hapa na tunashukuru kwamba wamefanikiwa” alisema Ipyana.

Alisema lengo lao kuu hasa Ni kuwaandaa watoto na vijana ambao watakiwa Ni wabunifu na kuweza kutatua changamoto mbalimbali kwa kupitia yale amabayo walishayasoma darasani ikiwemo Yale ambayo yanawazunguka katika mazingira wanayoishi.

Dhima kubwa Ni kuhakikisha tunatengeneza vijana ambao ni wabunifu na kuweza kutatua changamoto mbalimbali kwa kupitia Yale ambayo wanayasoma darasani kwahiyo mafunzo haha yanahakikisha tunapata vijana wabunifu ambapo pia Wana uwezo was kufikiria zaidi ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo tabia nchi na zile ambazo zinawazunguka kwenye jamii yao” aliongeza Dk. Ipyana.

Akizungumza kwaniaba ya Botna Foundation Mbogolo Philoteus alisema shirika hilo linaamini kumuandaa kijana katika karne ya sasa na ijayo kwaajili ya kuingia kwenye soko la kiushindani hatua ambayo inasaidia kujiepusha kujiingiza katika mmomonyoko wa maadili na makundi maovu ambayo yanaweza kumfanya kutokutimiza ndoto zake kielimu, kijamii kisaiasa na nyanja mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!