Home Kitaifa WALEZI TIMIZENI JUKUMU LA ULEZI, MMOMONYOKO WA MAADILI UMESHIKA KASI

WALEZI TIMIZENI JUKUMU LA ULEZI, MMOMONYOKO WA MAADILI UMESHIKA KASI

Na Magrethy Katengu

Walezi wameshauriwa kuangalia watoto kwa ukaribu kwani kuna Mmomonyoko wa maadili na Vijana wameharibika wengine wakiwa wamejiunga na utumiaji dawa za kulevya, ukahaba usagaji na ushoga hali hiyo ni hatari kizazi kijacho .

Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati tukio la kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi Makabe Mlezi wa UVCCM tawi la Mabibo chuo kikuu cha pia ni Makamu Mwenyekiti wa Walezi wa vyuo vya kati na vikuu vya Mkoa wa Dar es salaam Dkt Benadecta Lushau ambapo amesema wamefanya hivyo ikiwa ni kuwakumbuka watoto waishio katika jamii iliyotuzunguka kwani kufanya hivyo watoto hao wanajisikia kuwa siyo wapweke

“Walezi kuanzia ngazi ya familia mashuleni na vyuoni tuone kundi hili kuwa ni watu pekee sana katika jamii kwani muda wanaokuwa na watoto huwapatia malezi mazuri ili kusaidia kuishi maisha mazuri na kuepuka na ushawishi wa kujiingiza na makundi yasiyofaa ikiwemo uvutaji bangi,wizi ukahaba mambo ambayo yanaathiri ukuaji na kukosa viongozi wazuri wa baadae” mesema Dkt Benadecta

Naye Katibu Mwenezi Makondeko Ubungo Mariam Mbegha amesema Agosti 19 ni siku yake ya kuzaliwa hivyo ameona ni vyema kuitumia siku hiyo kupika chakula kwenda kula pamoja na watoto hao yatima kwani kundi hilo kubwa lenye uhitaji hivyo kama mtu mmoja mmoja kadri Mungu alivyombariki ni vyema kama ana sherehe yake kuja kufurahi na watoto hao wanajisikia vizuri kuona nao wanathaminiwa na jamii iliyowazunguka .

Kwa upande wake Mlezi Msaidizi wa Kituo hiko Neema Yunusu ameshukuru kwa Ugeni ulifika katika kituo hiko kwani kituo chao kilianzia Magomeni Mikumi kikahamishiwa huku mwaka 2013 Mbezi Makabe wakiwa na watoto 21 na sasa wako 32 na wote wanasoma watoto 12 wako shule binafsi bodi na watoto 3 wamehitimu kidato cha 6 na 2 wako Jeshini kwa ajili ya mafunzo na 1 alikosa nafasi jeshini..

Naye miongoni mwa watoto hao Yatima Azal Masasu amesema yeye ni miongoni mwa watoto waliopata malezi katika kituo hiko mpaka amehitimu kidato cha sita hivyo wanashukuru kwa wadau wanaokuja kuwaona na kuwapatia misaada kwani wanakabiliwa na changamoto za vyakula wakati mwingine pia nauli za kwenda shuleni hasa wanafunzi wa Sekondari wanatembea umbali mrefu kwenda shule.

Aidha ameomba wadau wote watakaoguswa wanakaribishwa kuja kuwaona Mbezi Msakuzi kwani kuna uhitaji ukarabati wa jengo lao hali siyo nzuri na vijana wao wanaosoma wana mahitaji yao ikiewemo nauli za kwendea shuleni hasa wanafunzi wa sekondari pia vyakula kutoa ni moyo wala si utajiri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!