Home Afya WAGONJWA NCHI JIRANI WAKIMBILIA TANZANIA KUPATA HUDUMA ZA UBINGWA BOBEZI.

WAGONJWA NCHI JIRANI WAKIMBILIA TANZANIA KUPATA HUDUMA ZA UBINGWA BOBEZI.

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameanika mafanikio makubwa ya sekta ya afya bungeni jijini Dodoma leo, Mei 11, 2026, akibainisha kuwa Tanzania imekuwa kinara barani Afrika katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Katika wasilisho la bajeti ya wizara hiyo, Mchengerwa amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imeshuhudia anguko la kihistoria la vifo vya uzazi kutoka vifo 556 (mwaka 2016) hadi vifo 104 pekee (mwaka 2022) kwa kila vizazi hai 100,000 huku wodi za watoto wachanga zikiongezeka kutoka 80 hadi 438, na vituo vya upasuaji wa dharura vikifikia 630.

Aidha ameeleza kuwa nchi imepiga hatua kubwa katika tiba bobezi na teknolojia ya uchunguzi, hali inayoiweka Tanzania kwenye ramani ya “Tiba Utalii” (Medical Tourism) ambapo imefanikiwa kufanya upandikizaji wa figo 170, uloto 57, na upasuaji wa nyonga na magoti kwa wagonjwa 3,037 na jumla ya wagonjwa 26,770 kutoka nchi jirani wamekuja nchini kupata huduma za ubingwa, jambo linaloimarisha diplomasia na uchumi wa nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!