Home Kitaifa WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

OR – TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe ameungana na timu ya Ufuatiliaji wa Kisekta, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wadau wa Elimu nchini ili kufanya kufanya tathmini ya masuala ya elimu nchini.

Timu hiyo imekutana jana tarehe 19 Septemba, 2022 jijini Arusha kwa lengo la kufanya tathmini ya kina kuhusu matumizi ya TEHAMA katika shule za msingi na sekondari.

Prof Shemdoe anaendelea kufafanua kuwa tathmini hiyo itawahusisha wanafunzi, walimu, wazazi na kamati pamoja na Bodi za shule kwenye shule zinazo tumia TEHAMA na zile ambazo hazitumii ili kuona kama kuna manufaa ya matumizi ya TEHAMA kwenye kuboresha Elimu na ujifunzaji.

Ametoa wito kwa shule na wadau watakao tembelewa kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi ili kuiwezesha Serikali kuona namna bora ya kuboresha namna ya ujifunzaji katika shule za Umma.

Kabla ya kuanza vikao hivyo vya tathmini, Prof Shemdoe alikutana na Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, hasa kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha wanapeleka fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo ili ziwanufaishe wananchi.

Pia amewasisitiza wajumbe wa Menejimeti ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na Mamlaka nyingine za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanajibu hoja za ukaguzi na kwamba suala la ukusanyaji wa mapato na kujibu hoja za ukaguzi ziwe agenda za kudumu katika vikao vuao.

Prof. Shemdoe amewaelekeza wajumbe wa Menejimenti hiyo kuwa watumishi wanapohamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine si adhabu bali wanahamishwa kwenda kuongeza nguvu ya utendaji kwenye kituo kingine ili kuwatumikia wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!