Home Kitaifa Veta Yatunuku Vyeti Vya Ujuzi Kwa Wafungwa 481

Veta Yatunuku Vyeti Vya Ujuzi Kwa Wafungwa 481

Celebrating 25 Years of NHIF

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetunuku vyeti vya Urasimishaji Ujuzi kwa wafungwa 481 waliokidhi vigezo pitia programu ya Mama Samia ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi.

Hafla kutunuku vyeti imefanyika , tarehe 25, Novemba, 2026 katika viwanja vya Gereza Karanga mkoani Kilimanjaro ikiambatana na utiaji saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya VETA na Jeshi la Magereza iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore na Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Kamisha Jenerali (CGP), Jeremiah Yoram Katungu.

FAHARI AFYA

Kwamujibu wa hati ya makubaliano, ushirikiano huo umelenga Kutambua, Kuthibitisha na Kurasimisha ujuzi wa wafungwa ili kuwawezesha kutumia ujuzi watakaoupata kujiajiri au kuajiriwa wanaporejea katika jamii.Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema kurasimisha Ujuzi ni moja ya nyenzo za utekelezaji Dira 2050 , ambayo inalenga kuandaa na kuwajenga wananchi uwezo wa kutumia ujuzi wao kujipatia kipato na kuinua uchumi wa Taifa.

“Fanyeni tathmini kwa lengo la kuboresha zaid mafunzo ili yaendane na soko la ajira na kuimarisha uwezo wa wanafunzi katika kujifunza,” ameelekezaKwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Muship amesema amepongeza mpango wa kurasimisha ujuzi kwa wafungwa, kwani unawezesha kuongeza tija ya ujuzi wa wafungwa na kuwawezesha kujitegemea.Akitoa salamu za VETA, Mkurgenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore VETA nashiriki moja kwa moja katika ujenzi wa msingi imara wa uchumi binafsi kwa wafungwa wanapokamilisha vifungo vyao.  

Naye Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Kamishna Jenerali Jeremia Yoramu Katungu, amesema ushirikiano na VETA katika kutoa ujuzi kwa wafungwa utawasaidia watakapomaliza vifungo vyao na kurejea mtaani wataweza kujiajiri,kuajiriwa na kuajiri wengine na hivyo kuleta tija.

Akitoa taarifa kuhusu zoezi la Urasimishaji Ujuzi kwa Wafungwa, Mratibu wa Programu ya Mama Samia ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi, Richard Mwakapeje, amesema wafungwa 481 wamekidhi vigezo katika fani 11 ambapo wanaume ni 428 na wanawake ni 53.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!