Home Kitaifa USHIRIKIANO WA TANZANIA NA JAPAN WAIMARISHWA KUPITIA TRA

USHIRIKIANO WA TANZANIA NA JAPAN WAIMARISHWA KUPITIA TRA

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, leo tarehe 03 Januari 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.

Katika mazungumzo yao, yaliyojikita kwenye masuala ya kodi, uwekezaji, kubadilishana uzoefu na biashara, Balozi Misawa ameipongeza TRA kwa kufanya makusanyo makubwa ya kodi kwa njia ya kistaarabu, jambo ambalo linachochea uwekezaji.

Balozi Misawa amesema wataendelea kudumisha uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Japan kwa kushirikiana na TRA katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Aidha, Balozi huyo amegusia suala la kubadilishana uzoefu katika masuala ya kodi baina ya TRA na Mamlaka ya Mapato nchini Japan ili kuongeza ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema wanathamini uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya TRA na Japan katika masuala mbalimbali ya kikodi na uwekezaji.

Bw. Mwenda amesema zipo sheria zinazoiongoza TRA katika kushughulikia masuala ya kidiplomasia na uwekezaji, ambazo zimekuwa zikitekelezwa kikamilifu ili kuweka mazingira mazuri kwa ufanyaji biashara kimataifa na uwekezaji.

Tunaishukuru sana Serikali ya Japan kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania ambayo yamekuwa na manufaa chanya. Tunaahidi kama TRA tutaendeleza mahusiano hayo yenye tija kidiplomasia,” amesema Kamishna Mkuu Mwenda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!