Home Kitaifa TUNAOMBA ULINZI  KUELEKEA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU NCHINI....

TUNAOMBA ULINZI  KUELEKEA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU NCHINI. – MOLLEL

WATU  wenye Ulemavu  wa Ngozi Ualbino nchini  wameiomba serikali  kuwawekea mazingira ya usalama wao  katika kuelekea  kipindi cha  Uchaguzi  wa Serikali za mitaa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu  na Uchaguzi Mkuu ujao 2025.

Hayo  yamesemwa  na Mwenyekiti  wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino (TASS) Godson Mollel 
katika Kongamano  la Uelewa  kuhusu Ualbino  ambao kilele chake kimataifa ni June 13 kila mwaka.

Mollel amesema kipindi kipindi hiki tunapoelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani kundi hilo lihakikishiwe Ulinzi na usalama wao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha  Mkoa wa Pwani  Nickson Simon  amewatoa hofu Chama  Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) kwamba serikali itahakikisha inakomesha  vitendo vya  mauaji  kwa watu wenye changamoto  ya ngozi (Albino).

Serikali  iko kazini  katika kuzuia  mauaji  ya Albino  nchini  na kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji  Abubakari Kunenge ambaye amenituma nije kumuwakilisha katika Kongamano  hili leo nasema  kuwa vitendo hivi vitakomeshwa kabisa endapo tu tutatumia  njia ya kupeana  elimu kwani tunaimani kubwa endapo jamii  wakipata ufahamu  wa kutosha kwamba vitendo vya mauaji ya Albino ni kinyume  na haki za binadamu  na kwamba  watu wote tuna haki ya  kuishi kwa misingi   ya utu,undugu na amani mauaji  haya yatakoma.

Kitakwimu inaonesha kuwa kati ya watu 20,000 mtu mmoja anavinasaba vya Ualbino , kati ya watu1,400 mmoja kati yao ni Albino huku ndani ya Mkoa wa Pwani kuna watu 569 huku watu 368 ambao wanahudhuria Kliniki  na wanapata  misaada  mbalimbali  inayowahusu.

DC Nickson  amesema hayo  leo  wakati alipokuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika Kongamano la  Uelewa  kuhusu Ualbino  linalofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shule ya Siasa ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Kibaha  Mkoani Pwani.

Elimu zaidi  inahitajika  kwa jamii kuhusu kukwepa unyanyapaa dhidi ya  watu wenye ualbino na mauaji yatakoma pindi tu  jamii  itakapokuwa  na uelewa wa kutosha juu ya changamoto ya watu wenye Ualbino” amesema  DC Simon.

Aidha Mollel alipozungumza na waandishi wa habari baada ya maadhimisho hayo ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa watu wanaokutwa na hatia ya kuwakata viungo au kuwaua watu wenye, Mahakama ikitoa hukumu kali kwa wahusika wa mauaji ya Albino itakuwa fundisho kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha kuwadhuru.

Mkurugenzi wa Kitengo Cha Huduma kwa watu Wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri  Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu Wenye  Ulemavu Rasheed  Maftah amesema kwamba serikali  inaandaa sera na miongozo mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ili kuweka usawa.

Wakati huohuo Ofisa  Ustawi Mkuu  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Joy Maongezi amesema kuwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 inataka kuwa na haki kwa watu wenye ulemavu ambapo watu wenye Ualbino ni sehemu yao.

Katika maadhimisho hayo  huduma mbalimbali zimetolewa ikiwa ni pamoja na upimaji saratani ya ngozi, utoaji miwani, kofia na mafuta maalumu ya kuzuia ngozi kutoathirika  na  mionzi ya jua , upimaji wa tezi dume na kansa ya mlango wa shingo ya kizazi.

Maadhimisho hayo hufikia kilele  kila ifikapo Juni 13 dunia kote  na kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika Kibaha Mkoani Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!