Home Kitaifa TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKI WAKE KWENYE MIKUTANO YA KIKANDA NA KIMATAIFA

TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKI WAKE KWENYE MIKUTANO YA KIKANDA NA KIMATAIFA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akizindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024, wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70),leo Mei 9,2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na tija ya ushiriki wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.

Akizungumza leo Mei 9,2026 jijini Dodoma wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70), Dkt. Gwajima amesema  mwongozo huo umeandaliwa mahsusi kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji pamoja na tathmini ya ushiriki wa Serikali na wadau mbalimbali katika mikutano ya nje ya nchi.

Amesema hatua hiyo itawezesha Serikali kuwa na mfumo madhubuti wa kufahamu mikutano inayoshirikisha wadau wa maendeleo ya jamii, jinsia na wanawake, sambamba na kutathmini manufaa yanayopatikana kwa taifa kupitia ushiriki huo.

“Lengo letu ni kuhakikisha kila ushiriki wa Tanzania katika mikutano ya kikanda na kimataifa unakuwa na matokeo yenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla,” amesema Dkt. Gwajima.

Waziri Gwajima ameeleza kuwa mwongozo huo pia utaongeza uwajibikaji na ushirikishwaji kwa kuweka utaratibu unaoeleweka kuanzia hatua za maandalizi, ushiriki hadi tathmini baada ya mikutano kumalizika.

Aidha, amewataka viongozi wa Wizara kuhakikisha wadau wanashirikishwa tangu mwanzo wa maandalizi ya mikutano hiyo, ikiwemo katika uteuzi wa viongozi, wajumbe pamoja na kamati ndogondogo zitakazosimamia ushiriki wa Tanzania katika majukwaa mbalimbali ya kikanda na kimataifa.

Amesema , ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na wadau utasaidia kuongeza nguvu ya uwakilishi wa Tanzania na kuhakikisha sauti ya nchi inasikika kwa ufanisi zaidi katika ajenda za maendeleo ya wanawake, jinsia na makundi maalum duniani.

Hata hivyo amesema kuwa Tanzania inahitaji ushiriki wenye tija zaidi katika mikutano ya kikanda na kimataifa ili kuhakikisha masuala ya wanawake, jinsia na makundi maalum yanapata matokeo chanya kwa taifa.

Dkt. Gwajima amesema ni wakati sasa kwa wadau wote kushirikiana kwa karibu katika maandalizi, uratibu na tathmini ya mikutano hiyo ili kuongeza ufanisi wa ushiriki wa Tanzania duniani.

Amesema  mafanikio ya ushiriki wa kimataifa yanategemea maandalizi madhubuti yanayohusisha uandaaji wa ripoti za nchi, upatikanaji wa rasilimali fedha pamoja na ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo wanawake, vijana, wanaume, wazee, wajane na viongozi wa serikali waliopo na waliostaafu.”amesema Dkt.Gwajima

“Tunatakiwa kujipanga kama timu moja kuhakikisha ushiriki wetu unaendana na kaulimbiu za mikutano husika na kuleta manufaa halisi kwa nchi,” amesema  Dkt. Gwajima.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi kutoka  Tanzania bara na Zanzibar,mashirika yasiyo ya kiserikali, wahandisi wanawake, majaji pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya jinsia na wanawake nchini kwa lengo la kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika mkutano wa CSW70 uliofanyika jijini New York, Marekani mwezi Machi mwaka huu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza leo Mei 9,2026 jijini Dodoma wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70),pamoja na kuzindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akisisitiza jambo  wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70),pamoja na kuzindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani)  wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70) ulioenda sambamba na kuzindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akizindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024.hafla iliyofanyika leo Mei 9,2026 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akizindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024,hafla iliyofanyika leo Mei 9,2026 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima,akionyesha  Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024 mara baada ya kuuzindua  leo Mei 9,2026 jijini Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!