Home Kitaifa T-PESA APP YAZINDULIWA

T-PESA APP YAZINDULIWA

Na Magrethy Katengu

KAMPUNI ya Simu ya TTCL imezindua huduma ya T-PESA APP ambayo itawarahisishia wateja wa mtandao huo kupata huduma mbalimbali za malipo kwa kutoa na kutuma mitandao yote popote walipo .

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde katika Maonyesho ya bishara sabasaba amesema huduma hiyo ni miongoni mwa maboresho makubwa waliyoyafanya ili kuwarahisishia wateja wao kufanya huduma mbalimbali kwa haraka zaidi.

“Kampuni ya T-PESA imeendelea kujikita kidigitali zaidi kwa kuzindua leo huduma ya T-PESA APP. Huu ni mfumo rahisi wenye ufanisi kwa wateja wanaotumia huduma za T-PESA,” amesema” Mkurugenzi huyo wa T-PESA.

Hata hivyo amesema kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kufanya malipo mbalimbali popote walipo na kwa haraka zaidi, ikiwemo kulipia bili za maji, umeme, ving’amuzi na faini mbalimbali za Serikali.

Hata hivyo amebainisha kuwa huduma hiyo inaenda kuwarahisishia kazi mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwani sasa kwa kutumia T-PESA APP wataweza kulipia viingiio vya mechi mbalimbali za mpira kwa NCARD.

Huduma ya QR Code ni njia ya haraka na rahisi ya kufanya malipo ambayo kwa T-PESA APP inawezekana katika maduka, migahawa na maeneo mbali mbali nchini ikiwemo vituo vya petrol vya Puma. Wateja pia wanaweza kuangalia salio bure, kununua au kutuma muda wa maongezi,” amesema.

Watanzania na Wateja kwa ujumla waneshauriwa kuendelea kutumia huduma za T-Pesa na kama bado hawana laini za TTCL basi wajisajili mara moja ili kufurahia huduma kwa bei nafuu.

Huduma hii ya T-PESA APP inapatikana kwenye ANDROID kwa kupakua kupitia google playstore Tunajivunia huduma hii kwani T-PESA APP ni tofauti na APP nyingine za mitandao ya simu kwa sababu ina huduma ya kipekee ya kumuwezesha mteja wetu kununua tiketi za mpira wa miguu kwenye mechi zote zinazochezwa Tanzania Bara,” aliongeza Bi. Mkudde.

Amesema Kampuni ya T-PESA itaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta mbalimbali ili kuondoa changamoto zilizopo na kuendana na matumizi ya mifumo ya kidigitali na kupelekea upatikanaji wa huduma zake kwa wakati na urahisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!