Home Kitaifa SHULE ZA SEKONDARI 19 KUJENGA MAABARA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

SHULE ZA SEKONDARI 19 KUJENGA MAABARA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

SHULE 19 za sekondari za Kata katika jimbo la Musoma vijijini zinaendelea na ujenzi wa maabara kwaajili ya ugundishaji wa masomo ya sayansi.

Maabara hizo zinajengwa kwa michango ya wanakijiji kwa kushirikiana na serikali na mchango wa mbunge wa jimbo hilo,Prof.Sospeter Muhongo.

Wanavijiji wa jimbo la Musoma vijijini wamedhamiria kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zao za Kata za masomo ya fizikia, kemia na baiolojia.

Jimbo hilo lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya sekondari 25 za Kata, na 2 za binafsi.

Katika ujenzi wa maabara hizo nguvukazi za Wanavijiji kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga, maji na kuchimba misingi ya majengo zimekuwa zikitumika.

Akizungumzia maendelep ya ujenzi wa maabara hizo mbunge wa jimbo la Musoma vijijini amesema licha ya michango hiyo zipo fedha kutoka mfuko wa jimbo, eerikali kuu kupitia Tamisemi na Wizara ya Elimu.

Amesema pia wadau wa maendeleo zikiwemo benki za NMB, CRDB, NBC na TCB na baadhi ya wazaliwa wa vijiji vinavyofanya ujenzi wamekuwa wakichangia.

Muhongo amesema sekondari zenye maabara 3 za masomo ya sayansi zilizokamilika na zinazotumika ni Mugango iliyopo Kata ya Mugango, Bugwema, Kata ya Bugwema, Kiriba, Kata ya Kiriba, Nyakatende, Kata ya Nyakatende, na Ifulifu, Kata ya Ifulifu.

Aidha Makojo Sekondari ya Kata ya Makojo itakamilisha maabara ya tatu kabla ya julai 30 mwaka huu na kuanza kutumika

Ameongeza kuwa sekondari 4 mpya zinazojengwa Nyasaungu, Muhoji, Wanyere na Rukuba Kisiwani lazima majengo ya maabara 3 za masomo ya sayansi yawe sehemu ya ujenzi wa maabara.

Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushawishiwa na kuombwa nayo ianze kuchangia kwa kutumia mapato yake ya ndani ujenzi wa maabara na maktaba kwenye shule zetu”

Masomo ya hisabati na sayansi kwa ngazi ya awali ya shule za msingi na sekondari ndiyo msingi imara wa taaluma mbalimbali za kiufundi zinazotoa kwa uharaka ajira ndani na nje ya nchi” amesema.

Wanafunzi wa sekondari za Kata za Musoma Vijijini, wazazi na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu jimbo la Musoma vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!