Home Kitaifa SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) LIMEWATAKA WAZALISHAJI NA WAINGIZAJI WA BIDHAA NCHINI...

SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) LIMEWATAKA WAZALISHAJI NA WAINGIZAJI WA BIDHAA NCHINI KUSHIRIKIANA NAO

Shirika la viwango Tanzania,(TBC) limewataka Wazalishaji na waingizaji wa bidhaa kushirikiana nao kwa lengo la kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini unazingatiwa ili kusaidia katika kulinda uchumi wa nchi na kupunguza hasara kwa wafanyabiashara.

Hayo yamesemwa na Mkaguzi kutoka kitengo cha Bidhaa zinazotoka nje ya nchi (TBS), Bw. Andalalisye Mwakyonde leo Novemba 25,2022 Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wamefanya ziara katika Makao Makuu ya TBS Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa bidhaa inayotokea nje ya Nchi lazima ikaguliwe kwanza kabla ya kusambaza kwa lengo la kupunguza gharama za ziada kwa muingizaji, husaidia utoaji wa mizigo kwa haraka bila ya kukutana na changamoto mbalimbali.

Bidhaa yoyote inayotokea nje ya Nchi lazima ikaguliwe kwanza kabla ya kusambaza kwa wananchi na kupewa conditional release ambacho ni kibali Cha masharti kinachomruhusu mteja kusambaza bidhaa zake“amesema Mwakyonde

Aidha Afisa Usalama wa Chakula Mkuu TBS, Bi. Coletha Sarimbo amesisitiza umuhimu wa usajili wa bidhaa hususani za chakula na vipodozi katika kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa husika ili kulinda afya za watumiaji na vilevile kusaidia wananchi kupata taarifa sahihi ya bidhaa kulingana na viambata vilivyopo kwenye bidhaa hizo.

Bi.Sarimbo alitoa wito kwa wafanyabiashara wanaoandaa matangazo yanayohusu vyakula na vipodozi kuyawasilisha TBS kwa ajili ya mapitio na baadae kupewa kibali ili kuhakikisha matangazo hayo hayamrubuni mlaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!