Na Magrethy Katengu
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimepongezwa kwa kuwakamata watu watatu akiwemo Balozi Mstaafu Willibroad Silaa,Bonfase Mwakumbusi na Mdude Nyangali kwa kosa la kuhamasisha wananchi kufanya maandamano ya kuipindua Serikali ya awamu ya Sita inayoendeshwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani .
Pongezi hizo amezitoa Jijini Dar es salaam na Katibu ws Baraza la habari la Kiislam( BAHAKITA) Sheikh Mwaipopo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema watanzamia wanatakiwa kutambua kuwa kukamatwa kwa watu hao walikuwa wanakwenda kusababisha nchi kuingia katika machafuko vyombo vya ulinzi na usalama viko vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria hawakuonewa nanaendelea kuhojiwa.
“Kwa mijibu wa Jeshi la polisi Wakili Bonifase Mwakumbusi na Mdude walikamatwa Agosti 12 ,2023 Mikumi Mkoani Morogoro,huku Balozi Mstaafu Willibriad Slaa akikamatwa Agosti 13,2023 Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kutoa kauli za kichochezi ambapo ni kosa kisheria” amesema Sheikh
Sambamba na hayo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakitoa lugha mbalimbali katika mikutano yao ya hadhara kwa kusema wataendesha maandamano nchi nzima wakianzia Dodoma, Dar es salaam kupindua serikali illyopo madarakani kabla ya mwaka 2025 hivyo baada ya kuwekwa chini ya ulinzi mkali na jeshi la.polisi na kukutwa na kesi ya uhaini hivyo wananchi wamesisitizwa Jeshi limefanya hivyo ili kuiweka Tanzania tunu ya amani iliyopo isipotee.
Hata hivyo ameshangazwa na baadhi ya viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kujichanganya wakati siyo majukumu yao kwani wao wanatakiwa wawaombee watu kutoka katika tambia mbaya na kuwa na tabia njema lakini hivyo kabla ya kujichanganya na wanasiasa wajitathimini kwanza maana nao wanaweza kuingia katika mikumbo isiyowahusu.








