Home Kitaifa SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANAKIJIJI KUFUNGULIWA MWEZI HUU MUSOMA

SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANAKIJIJI KUFUNGULIWA MWEZI HUU MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kijiji cha Muhoji jimbo la Musoma Vijijini kimeamua kujenga sekondari yake ili kutatua tatizo la umbali mrefu wanaotembea watoto wa kijiji hicho kwenda masomoni kwenye sekondari ya Kata iliyoko Kijiji cha Masinono umbali wa zaidi ya kilomita kumi (10)

Ujenzi ulianza kwa kupitia harambee za mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo ambae anachangia fedha zake binafsi.

Mfuko wa jimbo unachangia baadhi ya vifaa vya ujenzi,wanakijiji wanachangia fedha za ujenzi na nguvukazi zao.

Wanakijiji wa Muhoji wamemshukuru mbunge Muhongo kwa jitihada zake ambazo zimepelekea kupatikana kwa shule hiyo.

Wamesema umbali waliokuwa wakitembea mrefu waliokuwa wakitembea watoto ilikiwa ikipelekea kutokusoma kwa ufanisi.

Wakati wananchi wakitoa shukrani hizo ofisi ya mbunge imetoa taarifa na kudai serikali imeanza kuchangia ujenzi wa sekondari hiyo kwa kutoa shilingi milioni 75 na kuishukuru

Muhoji sekondari ipo tayari mwezi huu kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka kijijini humo.

Sekondari hii mpya kwa miaka ya karibuni itapokea wanafunzi kutoka vijiji jirani vya Kaburabura (Kata ya Bugoji), Saragana (Kata ya Nyambono) na wanafunzi kutoka Wilaya ya Bunda, Kitongoji jirani cha Kinyambwiga.

Taarifa hiyo imesema majengo yaliyokamilishwa vyumba vya madarasa vitatu (3),ofisi moja,vyoo matundu 8,chumba cha maktaba na chumba cha huduma ya kwanza.

“Michango bado inahitajika wa
ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye sekondari hii mpya ikiwemo maabara tatu za masomo ya sayasi, vyumba vipya vya madarasa, na nyumba za walimu.

” Tujitahidi kuwekeza kwenye elimu kwa kuchangia ili malengo tunayo kusudia kwenye suala la elimu yaweze kufanikiwa”,imesema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!