
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Lomatan, Loveness Edwin Mamuya amewaongoza Watanzania katika kampeni ya kupiga vita pombe feki na haramu, akisisitiza kuwa unywaji wa vinywaji visivyokidhi viwango ni uhujumu wa afya ya jamii na nguvu kazi ya taifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jioni ya Ijumaa Aprili 24, 2026, wakati wa uzinduzi wa chapa ya Riviera, Loveness amesema uzalendo wa dhati ni kulinda afya ya vijana wa Tanzania.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga kama mgeni rasmi, Loveness amewataka Watanzania wote kujiunga na Waziri Judith Kapinga kutoa taarifa na kukataa vinywaji hivyo vinavyopoteza kizazi cha vijana.
“Kama Mtanzania hii ni brandi ya kwanza ya mwanamke Mtanzania, Afrika Mashariki. Kwahiyo, tunaomba sisi wanawake, sisi, si ndio mama, mtoto akinywa pombe feki akiharibika maana yake ni nini? Anamuumiza mama. Sasa sisi wamama tukaibebe Lomatan, tukaibebe Jagaboom ili kila mtoto wetu tumkumbushe, ‘usinywe pombe feki ni tatizo kwa afya yako’”, ameeleza Loveness.

Amesema bidhaa mpya za Riviera zimetayarishwa kwa utaalamu wa hali ya juu kutoka nchini Ujerumani (Germany) ili kuhakikisha usalama na ubora wa hali ya juu kwa mtumiaji.
Bidhaa nne zilizoingizwa sokoni kwa brandi ya Riviera ni Jagaboom, Lomatan Whiskey, Lomatan Gin na Lomatan Vodka








