Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya, amepongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), hususan hatua ya kuanzisha mpango wa kuuza mifugo kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Akizungumza alipotembelea banda la WRRB katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea viwanja vya John Malecela jijini Dodoma leo Agosti 2, 2026, Wambuya amesema “Niwapongeze sana, kwa kazi nzuri mnayofanya, nimeona mpango wenu kuingiza mifugo kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, natumai mpo hatua nzuri kwasasa.”
Kwa upande wake, Ofisa Leseni wa WRRB, Nasri Khea, amesema maandalizi ya mnada wa kwanza wa mifugo kupitia Mfumo huu yamefikia hatua za mwisho, huku mnada huo ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni katika Wilaya ya Mvomero.
Amesema pia mfumo huo unakwenda kuingiza kuwezesha biashara za bidhaa mbalimbali ikiwamo Mwani na mahindi.














