
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, ameshiriki zoezi la upigaji kura katika Mtaa wa Bombambili, Mjini Geita.
Akiwa kwenye shughuli hiyo, Manjale aliwasihi vijana kuwa watulivu katika kipindi chote cha uchaguzi na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani katika maeneo yao.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia huku wakizingatia misingi ya utulivu na mshikamano, ili kudumisha amani ambayo ni msingi wa maendeleo katika jamii.
Manjale alihitimisha kwa kuwapongeza vijana wote kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuonyesha uzalendo kwa taifa.