
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Chacha Wambura, ameshiriki zoezi la kupiga kura leo katika ofisi za Serikali ya Kata ya Bomba Mbili, Mjini Geita.
Zoezi hilo limefanyika kwa amani na utulivu, likiwa ni sehemu ya utekelezaji wa haki ya kidemokrasia kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chacha Wambura amepongeza maandalizi mazuri ya uchaguzi huo, akisema kuwa ni mfano mzuri wa jinsi demokrasia ndani ya chama hicho inavyoendelea kuimarika.

“Ni jukumu letu kushiriki kikamilifu katika michakato hii ili kuhakikisha tunalinda na kudumisha misingi ya chama chetu,” alisema MNEC Wambura baada ya kupiga kura.
Wanachama wa CCM katika eneo hilo wameonesha mwamko mkubwa, huku wakitoa hamasa ya mshikamano katika kukuza maendeleo ya kijamii na kisiasa kupitia ushiriki wa kila mmoja.