Home Kitaifa MUSOMA VIJIJINI KUMUENZI PROF.MASAMBA KWA UJENZI WA “DAVID MASSAMBA MEMORIAL SECONDARY SCHOOL”

MUSOMA VIJIJINI KUMUENZI PROF.MASAMBA KWA UJENZI WA “DAVID MASSAMBA MEMORIAL SECONDARY SCHOOL”

WANANCHI wa Kijiji cha Kurwaki jimbo la Musoma vijijini wamekubaliana kufanya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kumbuka gwiji wa kiswahili, Profesa Davidi Masamba.

Wakizungumza kwenye mazishi ya Profesa huyo wananchi hao wamesema kazi kubwa ya kuinua lugha ya kiswahili ni vyema kumkumbuka kwa ujenzi wa shule ya sekondari.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mukama Magesa amesema licha ya kuwa na sekondari kijijini hapo ni vyema kujenga sekondari ya pili.

Amesema sekondari hiyo itakuwa kumbukumbu nzuri ya kumkumbuka Profesa Masamba na haiwezekani akaondoka na jina lake likafutika.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Kurwaki kwa uamuzi walioufanya.

Amesema kwa mazuri aliyoyafanya Profesa Masamba hasa kwa kuinua lugha ya kiswahili na uamuzi wa kumuenzi kwa ujenzi wa shule ya sekondari ni uamuzi sahihi.

Muhongo amesema wataalamu wenzake wa lugha ya kiswahili wakiwemo wanafunzi wake wamemzungumzia marehemu kuwa alikuwa gwinji na Mbobezi kwenye eneo la, “Fonolojia ya Kibantu” – hayupo mwingine tena wa kariba yake.

Musoma vijijini wameamua kumuenzi marehemu Prof. David Massamba, kwa kujenga sekondari mpya kijijini kwao itakayopewa jina lake na kuitwa, “David Massamba Memorial Secondary School.” Ambapo ujenzi utaanza mwezi ujao septemba 2023.

“Nawashukuru wananchi kwa uamuzi huu na niwaombe familia ujenzi utakapoanza tushiriki kwa pamoja na muwe mnakuja huku kijijini kushiriki” amesema Profesa Muhongo.

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa. Hii ilikuwa sehemu ya matukio ya leo kwenye maziko ya Prof David Massamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!