Na Theophilida Felician Kagera.
Mzee Novati Joseph Mwijage Mkazi wa Mtaa wa Nyakanyasi Kata Bakoba Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ambaye ni mlemavu wa kutokuona anayejishughulisha na kazi ya kuponda kokoto nyumbani kwake amemuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassani kumshika mkono kwa kumwezesha vifaa mbalimbali vya kumsaidia kuzalisha kokoto nyingi zitakazosaidia kukidhi mahitaji ya familia yake.
Novati akizungumza hayo na Blog hii baada yakufika nyumbani kwake kuyashuhudia majukumu yake ya kuponda kokoto amesema kuwa kazi hiyo aliianza mnamo mwaka wa (2020).
Mlemavu huyo awali ameeleza kuwa alizaliwa mwaka (1972) akiwa salama na macho yake ya kiwa yanaona vizuri bila ya kasoro yoyote hivyo mwaka (1980) alipatwa na tatizo la kuumwa macho yake hatimaye ya kapofuka jumla licha yakupelekwa Hosptalini bila ya mafanikio yakuuona tena mwanga wa Dunia.
Ameendelea kueleza kuwa mwaka (1982) alianza kusoma shule ya Mgezamseto iliyopo Manispaa ya Bukoba na mwaka (1989) akamaliza dara la saba na mwaka (1998) akoa mke ambaye wameishi wote na kufanikiwa kupata watoto wa 8.

Mzee Novati mwenye umri wa Miaka 51 licha kuwa mlemavu wa kutokuona amekuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali kwa malengo ya kutafuta riziki ya familia yake ambapo amezitaja kazi alizozifanya kipindi cha nyuma ni pamoja na kuuza kuni, kutembeza nyanya, mayai, nyama ya mbuzi na nyinginezo.
Amefafanua kuwa katika kazi hizo alikumbana na changamoto za aina mbalimbali mitaani.
“sikumo moja nikiwa natembeza mayai mabichi nilijikwaa barabarani na kuanguka chini mayai yote yalivunjika kwa bahati mbaya zaidi yalikuwa ya mtu hivyo nilijikuta nikihaha namna ya kumlipa muhusika na baada ya kumlipa niliacha kabisa kutembeza mayai mabichi badala yake ni kaanza kutembeza yaliyopikwa” ameeleza Novat Joseph.
Baada kufanya kazi hizo kwa muda mrefu amesema kuwa zilimsaidia kupata kipato kidogo kidogo kilichokuwa kikimsaidia mahitaji ya familia hususani chakula nguo sambamba na kusomesha watoto wake.
Mwaka (2020) wazo lika mwingia la kuanza kazi yakuponda kokoto hivyo alianza kazi hiyo nyumbani kwake ambapo amekuwa akizikutana changamoto kadhaa ikiwemo ya ugumu wa kupata mawe kwa ukaribu, kuponda mawe kwa kutumia vifaa duni ikiwemo nyundo ndogo hali inayompelekea kushindwa kuzalisha kokoto kwa wingi, kutokupata wateja kwa wakati wakununua kokoto zake na nyinginezo rukuki
“Niliona nijikite katika kazi hii ili pengine inisaidie kuongeza kakipato make nina familia nina mke na watoto 8 mwanangu amemaliza kidato cha nne mwaka jana anatarajia kwenda kusoma chuo hapa na hangaika nione kama ntafanikiwa chochote cha kumsaidia mwanangu japo napata ugumu sana kwenye kazi hii wakati mwingine najiponda vidole nikiwa na ponda mawe haya lakini nafanikiwa kidogo kidogo ni kuombe Mama yetu Mpendwa Rais wetu Samia kisikie kilio changu hiki nishike mkono Mama kwakunipatia vifaa wezeshi ikiwemo Mashine yakuzichakata kokoto ili nizalishe kwa wingi na kwa tija” Mzee Novati akihadithia kwa msistizo.
Amefafanua kuwa kwa siku akiwa na mawe mazingira ya karbu huzalisha kokoto zaidi ya karai 10 kwa kumi na 15 ambapo bei yake ya kawaida kwa kila karai ni Sh 500 ila yeye hujikuta akiziuza kwa bei ya chini ya Sh 300 kutokana na baadhi ya wateja huzifuata kwake wenyewe na kupekelea kumilipa hiyo kwa sababu ya makato ya kuzifuata ila anapobahatika kuziwafikishia maeneo yao humlipa Sh 500 kiasi ambacho kinakuwa bado hakitoshelezi mahitaji ya familia yake.
Ameishukuru Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa namna anavyoendelea kuwatambua kwa vitendo watu wenye ulemavu hapa nchini hasa hasa kuunda wizara inayohusika nao moja kwa moja kwani hilo limekuwa ni faraja kwao litasaidia kuwainua zaidi kimaendeleo na kuzitatua changamoto zinazowakabili.
Amehitimisha akitoa wito kwa watu wenye ulemavu kutokukata tamaa badala yake wajikubali na kuongeza mapambano ya kujishughulisha na shughuli za kuwaingizia kipato kama ilivyo kwake yeye.

Evelina Juliusi ni mke wa Mzee Novati amesema kuwa anamshukuru mume wake kwa jinsi anavyopambana huku na kule katika kuwatafutia riziki ikiwemo hiyo ya kuponda kokoto” mume wangu anazikutana changamoto sana akiwa anaponda kokoto hizi mimi na watoto humsaidia kumsogezea mawe karibu kutoka mlimani ili aweze kufanya kazi yake vizuri lakini bado ni tabu tupu tunaishi hivyo hivyo ona mwanetu anatakiwa kwenda masomoni chuoni lakini mpaka sasa hatujapata mwelekeo wakupata pesa ya kumpeleka shule niiombe Serikali na wadau waweze kumsaidia mume wangu kwa chochote cha kumwezesha kufanya kazi yake kwa ufanisi ili azalishe zaidi ya hiki” amesema Mke wa Novati Evelina Juliusi.

Naye Mtoto wa Mzee Novati Nabos Novati mwenye umri wa miaka 20 amehitimu masomo ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Kagemu mwaka (2022) ameeleza kwamba baba yake licha ya kuwa mlemavu amepambana vikali katika kutafuta mahitaji ya kumsaidia mahitaji ya shule hatimaye akamaliza salama na kufaulu kwenda chuo japo anawaza sana namna itakavyopatika ada ya kumwezesha kwenda masomoni japo baba yake anaendelea kukaza kamba katika utafutaji wa pesa kwenye kazi yake ya kuponda kokoto.
Kijana Nabos ameiomba Serikali pamoja na wadau wengine kuwiwa na kumshika mkono katika kumchangia ada ya kumsaidia kwenda kuanza masomo yake ya chuo ndani ya mwaka huu.








