Na Shomari Binda-Musoma
MEYA wa Manispaa ya Musoma na diwani wa Kata ya Makoko Kapteni mstafu Patrick Gumbo ameongoza harambee kukamilisha ujenzi wa madrasa kufundishia watoto kwenye Msikiti wa Mwisenge uliopo Kata ya Kamnyonge.
Harambee hiyo ameiongoza leo januari 11 kwenye kisomo cha Maulid kilichofanyika Msikitini hapo na kuhudhuriwa na watu mbalumbali.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee hiyo amesema suala la elimu ya dini kwa vijana lina umuhimu mkubwa hasa kupatika eneo sahihi la kuipatia elimu hiyo.
Amesema katika madrasa kunafundishwa maadili mema na kumjua Mwisenge hivyo watoto wakiandaliwa kitapatikana kizazi bora.
Gumbo amesema kuchangia katika dini kuna faida kubwa kesho mbele za Mungu na jamii isijikite zaidi kuchangia katika dunia.

” Nimepata mualiko wa muda mfupi kutoka kwa Shekh Amani na nimekutana na jambo jema naomba tuungane kulikamilisha.
” Mimi nipo dini tofauti lakini katika suala la maendeleo na kuwajenga watoto kiimani tutashirikiana kwa pamoja”,amesema.
Kwa upande wake Shekh wa Msikiti wa Mwisenge Amani Kapama amesema jitihada zinafanyika katika dini kupitia Madrasa na ni vyema kuwa na madrasa za kufundishia.
Amesema tayari waumini na waislam wa Msikiti huo walishaanza ujenzi na jengo la madrsa lipo kwenye hatua za ukanilishaji.
Katika harambee kiasi cha shilingi milioni 3,2,65000 zikichangwa ikiwa ni fedha taslim na ahadi huku Meya Gumbo na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo wakichangia shilingi milioni 1,171,000