Home Kitaifa MAFUNZO YA WATENDAJI CCM RORYA YADAIWA KUVURUGWA NA MWENYEKITI WA CHAMA NA...

MAFUNZO YA WATENDAJI CCM RORYA YADAIWA KUVURUGWA NA MWENYEKITI WA CHAMA NA MBUNGE

Na Shomari Binda

MAFUNZO ya watendaji wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Rorya yamedaiwa kuingiliwa na kuvurugwa na viongozi wa chama hicho.

Viongozi wanaodaiwa kuvuruga mafunzo hayo ni mbunge wa jimbo la Rorya Jafari Wambura Chege na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya Ongujo Wakibara wakidaiwa kuingilia semina ya makatibu wa matawi na kata leo 20/02/2025 na kugawa posho shilingi 50,000 kwa kila katibu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mitandaoni ukiwa ni pamoja na group la Whassap la CCM mkoa wa Mara zimedai utaratibu huo unakiuka maelekezo kutoka makao makuu ya chama

Taarifa hiyo inadai kuwa mafunzo hayo ya watendaji yasiingiliwe na viongozi au wanasiasa kwa sababu ni mafunzo ya kiutendaji na chama kilisema kitagharamia kila kitu ikiwemo chakula na posho.

“Lengo la chama kufanya hivyo ilikuwa ni kuondoa urasim wa wagombea kutumia nafasi hiyo kutoa rushwa kinyume chake mwenyekiti wa chama na mgombea wake ambaye ndie mbunge kwa sasa wamevamia ukumbi na kutoa posho hizo.

“Jambo hili halijawafurahisha hata wakufunzi haswa kauli za Mwenyekiti na mbunge baada ya kuzuiwa na wakalazimisha kufanya kwa nguvu”,imesema sehemu ya taarifa.

Mzawa Blog imefatilia taarifa hiyo na kuzungumza na mbunge wa jimbo la Rorya Jafar Chege kwa njia ya simu na kudai yupo msibani toka asubuhi na hajaudhuria kikao hicho na kushangazwa na taarifa hiyo.

Chege amekili kuiona taarifa hiyo na kudai inasambazwa na mmoja wa watumishi wa serikali na sijui lengo lake”amesema

” Nimeshangazwa na taarifa hiyo mimi nipo msibani na nimeambiwa kikao hicho kimeenda vizuri na kimalizika salama hizo taarifa ni za uongo”,amesema Chege.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya Ongujo Wakibara hakuweza kupatikana kwenye simu na jitihada za kumtafuta kuzungumzia jambo hili zinaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!