Home Kitaifa MABASI YATOAYO HUDUMA YA USAFIRISHAJI ABIRIA MIKOANI YARUHUSIWA KUSAFIRI MASAA 24

MABASI YATOAYO HUDUMA YA USAFIRISHAJI ABIRIA MIKOANI YARUHUSIWA KUSAFIRI MASAA 24

Na Magrethy Katengu

Mabasi yanayotoa huduma ya usafirishaji abiria kwenda Mikoani yameruhusiwa kusafiri masaa 24 kutokana na hali ya Ulinzi na usalama kuboreshwa barabarani kote kwa kuwa na doria ya mara kwa mara

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kamishana wa Operesheni na Mafunzo Juma Khaji amesema utaratibu huo mpaya umekuja ikiwa ni Agizo alilolitoa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa hivyo kama Jeshi watahakikisha wanaimarisha hali ya Ulinzi na Usalama kwa kufanya doria na operesheni mara kwa mara hususani katika maeneo korofi yanayotishia usalama wa abiria.

Natoa Agizo kwa Makamanda wote wa Polisi wa mikoa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na doria za mara kwa mara masaa 24 katika Barabara zote ili kuepusha ajali zisizo za lazima zinazochangiwa na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva kutozingatia alama za barabarani na kuendesha mwendo mkali” amesema Kamishna

Sanjari na hayo amesema hapo awali mabasi yalikuwa yanazuiwa kusafirisha abiria hususani nyakati za usiku kulingana na Muda hivyo kutokana na Jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya kihalifu vilivyokuwa vinatendeka hivyo na wataendelea kuhakikisha Usalama wa abiria wanaosafiri wasiwe na hofu hali ya Ulinzi na Usalama ni shwari

Sambamba na hayo amesisitiza Wamiliki wa vyombo vya Moto ikiwa Magari yao yatatembea masaa 24 bila kupumzika kuhakikisha kunakuwa na dereva zaidi ya mmoja katika gari moja kwani kutakuwa na ukaguzi kukagua dereva ambaye anapokezana na tingo wake kuendesha gari wakati hana leseni hivyo wasilaumu sheria kali itachukuliwa kwa dereva huyo ikiwemo kunyang’anywa leseni yake au kumfutia .

Hata hivyo amesema kuna Makampuni ya Magari ambayo ni vinara vya kusababisha ajali hivyo Wamiliki wamesisitizwa kabala ya kuondoa gari kituoni kulifanyia ukaguzi kwani haitaruhusiwa Magari mabovu kuingia barabarani kutoa huduma ya usafiri

Aidha Kimishna Juma amewaomba wananchi kufichua vitendo vyote vya kihalifu pale wanapoona dalili za viashiria vya uvunjifu wa usalama ikiwemo dereva kuendesha gari mwendo mkali au akiwa amelewa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!