TAASISI ya Lupus Awareness and Support (LASF), kwa kushirikiana na wadau wa muziki Micshariki wazindua wimbo ya “Shujaa 2” kama sehemu ya kuendeleza jitihada ya kuwafikishia ujumbe jamii kuhisiana na ugonjwa wa lupus na kuacha kuwanyanyapaa .
Akizungumza na Wanahabari Leo 03,2023 Jijini Dar es salaam wakati akizindua wimbo huo wenye maudhui ya kuhusu ugonjwa wa lupus Muwakilishi wa Taasisi ya Lupus Awareness and Support (LASF),Hajjrath Mohammed amesema kwa sasa anamiaka 17 anaishi na ugonjwa huo ambapo amekuwa akipata nafasi kwenye majukwaa mbalimbali katika jamii kuhakikisha jamii inapata uelewa juu ya ugonjwa huo ambao hauambukizi hivyo wameamua kutumia jukwaa la Sanaa katika kufikisha ujumbe kwa haraka, zaidi.
“Wimbo wa shujaa 2 ni mahususi kutoa ujumbe kwa jamii kuacha unyanyapaa na kutoa elimu zaidi kwa ugonjwa huo na pia tutaendeleakulitumia jukwaa la Sanaa tumeanza na wimbo kisha tutahamia kwenye filamu na Maigizokuhakikishajamii inapata uwelewa zaidi “.
Pia Hajjrath ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Afya kujikita katika kutoa elimu ya ugonjwa wa lupus kama magonjwa mengine yanavopata nafasi katika jamii kukumbushwa.
Nae Mkurugenzi shirika la Vijana wenye ulemavu (YOWDO) Rajab Mpilipili amesema wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kutoa taarifa mbalimbali na kuikumbusha jamii kuwa walemavu ni watu kama watu wengine na wanapaswa kushiriki katika kazi za kijamii.
Pia amesema kutokana na jitihada zinazofanyika na taasisi ya Lasaf kuhakikisha jami inakuwa na Uwelewa wa ugonjwa huo wameamua kutumia upande wa pili wa jukwaa la sanaa ambapo kwa sasa jukwaa hilo limekuwa likifikisha kwa haraka ujumbe kwa hadhira.
“Tunatambua mchango mkubwa kupitia Sanaa katika kuifikia jamii hivyo tumewiwa na sisi kutumia jukwaa hilo lengo ni kuendelea kuifikia jamii yetu kwa haraka na kusambaza uelewa wa ugonjwa huo .”
..Mwisho…








