Home Michezo KLABU YA YANGA YAPATA UBALOZI KAMPENI YA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

KLABU YA YANGA YAPATA UBALOZI KAMPENI YA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

Na Magrethy Katengu

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,na Makundi Maalumu Dkt Dorothy Gwajima ameviomba Vilabu vya Mpira kushirikiana na Taasisi mbalimbali kukemea Mmomonyoko wa Maadili unaosababisha kutokea vitendo vya ukatili wa kijinsi ikiwemo Ulawiti,Ubakaji,unyanyasaji Ili kusaidia kutokimeza kabisa.

Ombi hilo amelitoa Leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa kutambulisha balozi wa klabu ya Yanga kuhusika katika kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo amesema Vilabu vya Mpira ikiwemo Simba, Yanga, Azam, Kagera Sugar, KMC, Ruvu, Singida Big Stars timu hizi zimekuwa na ushawishi wa kubeba makundi mbalimbali hivyo wanauwezo kushawishi na kusambaza ujumbe wa kutokomeza vitendo vya ukatili.

“Klabu ya Yanga imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa na vilabu vingine vya Mpira kujihisisha Kwa kushirikiana na mashabiki na wanachama wao kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega kuhakikisha vitendo viovu vinavyotendwa miongoni mwa Jamii yetu vinapungua na kupotea kabisa hivyo wanafanya kazi njema ya Jamii”amesema Dkt Gwajima

Sanjari na hayo amefurahishwa na Klabu hiyo kushirikiana na Wasanii,wanamuziki na taasisi mbalimbali kutumia siku ya mpira wa Simba na Yanga Elimu inatolewa kuhusu athari na madhara yake kufanya waigizaji na waimba taraabu ambapo amesema amesema kumekuwa na matukio yanayotokea .

Naye Raisi wa Klabu ya Yanga Mhandisi Haris Saidy amesema watashirikiana na Wizara hiyo kuhakikisha kupitia timu yao wanaotoa Elimu kwa wanachama wao namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwani watoto ndiyo Taifa la kesho hivyo wanaotenda vitendo hivyo lazima wawajibishwe kisheria

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!