Home Michezo KAWAIDA AHITIMISHA MICHUANO YA SAMIA CUP JIMBO LA SAME MASHARIKI…

KAWAIDA AHITIMISHA MICHUANO YA SAMIA CUP JIMBO LA SAME MASHARIKI…

NA ASHRACK MIRAJI SAME KILIMANJARO

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Mohamed Ally Kawaida (MCC), amehitimisha mashindano ya mpira wa miguu ya Samia cup jimbo la Same mashariki yaliyoshirikisha timu 91 ambayo yaliandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Anne Kilango Malecel.

Kawaida alisema kuwa, Mbunge Anne ameonyesha dhamira ya dhati ya kuinua vipaji vya vijana kwa kuanzisha mashinado hayo ambayo yalichezwa kwa mfumo wa kitarafa na hatimaye mabingwa kukutanishwa ili kushindana kijimbo na kumpata bingwa wa Jimbo.

Amesema kuwa, michezo inasaidia vijana kutojiingiza katika mambo maovu kwa kuwafanya kuwa bize na michezo na kuwataka wabunge kuiga mfano huo alioanzisha Anne Kilango Malecel.

Kwa upande wake, Mbunge Anne aliwataka Vijana wa jimbo hilo kuanza maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Hussein Mwinyi cup yanayotarajiwa kuanza Novemba mwaka huu.

Mbunge huyo amesema kuwa, lengo la kuanzisha mashindano hayo yaliyokuwa akichezwa kwa Tarafa tatu na badae jimbo ni kuwakutanisha vijana pamoja na kuwaonyesha jinsi ambavyo serikali ya awamu ya sita inavyosamini michezo .

Kawaida ameshuhudia fainali ya jimbo iliyozikutanisha timu kutoka kata ya Ndungu dhidi ya Kihurio ambapo Ndungu imeibuka mshindi kwa kuifunga Kihurio goli moja kwa bila.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!