Home Kitaifa KATIBU MKUU JAMAL KATUNDU AONGOZA KIKAO CHA USHIRIKIANO BAINA YA OFISI YA...

KATIBU MKUU JAMAL KATUNDU AONGOZA KIKAO CHA USHIRIKIANO BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA WIZARA YA KAZI KENYA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya walipotembelea Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), jijini Dar es Salaam tarehe 18 Aprili, 2023.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu (wa pili kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko (wa pili kutoka kulia) pamoja na watendaji kutoka Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) na wajumbe kutoka Wizara ya Kazi nchini Kenya.

Na; OWM – KVAU: DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu ameongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhamaji nguvu kazi, ukuzaji ujuzi kwa vijana, ukuzaji ajira na masuala mengineyo yanayohusu sekta ya kazi na ajira.

Akizungumza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa kikao hicho cha majadiliano kitafungua fursa kwa nchi hizo kushirikiana kwa karibu katika kubadilishana uzoefu juu ya  utekelezaji wa  majukumu sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko amepongeza namna ambavyo Ofisi ya Waziri Mkuu katika kukuza fursa za ajira, viwango vya kazi sambamba na kusimamia usalama na afya kwa wafanyakazi.

Aidha, Ujumbe huo umetembelea ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA). 

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko  anayesimamia masuala ya Kazi nchini Kenya. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!