Home Kimataifa KAMATI YA NJE YA BUNGE LA MAREKANI KUTEMBELEA TANZANIA

KAMATI YA NJE YA BUNGE LA MAREKANI KUTEMBELEA TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), anatarajia kufanya mazungumzo ya kina na viongozi wa Serikali pamoja na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani wakati wa ziara yake rasmi ya kikazi jijini Washington, D.C., nchini Marekani.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri atakutana na wadau mbalimbali muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao tayari amekutana nao ni Mbunge wa Chama cha Republican, Brian J. Mast wa Jimbo la Florida, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani. Katika mazungumzo hayo, walikubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Marekani pamoja na kupokea mwaliko wa Kamati hiyo kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!