Home Kitaifa JAJI MUTUNGI ;AVITAKA VYAMA VYA KISIASA KUACHANA NA MIGOGORO KUFANYA DEMOKRASIA YA...

JAJI MUTUNGI ;AVITAKA VYAMA VYA KISIASA KUACHANA NA MIGOGORO KUFANYA DEMOKRASIA YA KISTAARABU

Na Magrethy Katengu— Dar es salaam

Msajili wa vyama Vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kufuata sheria za usajili na katiba zao za vyama pale wanapofanya shughuli za ikiwemo uchaguzi wao wa ndani ili kuepukana na Migogoro inayoweza kuwasavabishia kuwa na makundi makundi na kujengeana chuki zisizokuwa na tija.

Agizo amelitoa leo Julai 9,2024 jijini Dar es Salaam na wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo, namna ya kuhimili migogoro inayotokea wenyewe kwa wenyewe pasipo kufikishana katika vyombo vya sheria .

Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa ni Taasisi hivyo vinapaswa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria ya nchi ili na wanapotenda Majukumu yao yawe yanatambulika .

“Haya Mafunzo ni mahusihusi na yamekuja kwa wakati muafaka yatasaidia kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo Mogogoro inayosababishwa ubadhilifu wa fedha za chama, matumizi mabaya ya madaraka au ofisi ambayo imekua ikiripotiwa mara kwa mara kwenye taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)amesema Jaji Mutungi.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa wao wanapenda kuona vyama miafaka pale kunapotokea jambo lolote kukaa meza moja na kufanya maridhiano ya pamoja hivyo ameshauri vyama vya siasa kuwa vinara wa kujenga nchi na kwani Tanzania sio nchi ambayo inapata utawala kwa mabavu bali ni demokrasia makini na sera kwa wananchi.

“Migongano ndani ya chama haina budi kutoke lakini mkiwa na desturi ya kukaa meza moja na kumaliza pasipo kujilikana hakika Mkifanya mema wafuasi wengi watawafuata,mkiwa na migogoro isiyoisha hakuna atakaewafuata jitahidini kulinda tunu ya Amani ya Taifa msiwe wachochezi wa kuivuruga” amesisitiza Jaji Mutungi

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha ACT – Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa migogoro ya vyama vya siasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya maridhiano na sio kutumia nguvu na mabavu .

“Ni kweli Migogoro inapasua vyama ,hivyo kupitia mafunzo haya tutakayopewa tutajifunza kutatua migogoro kwa njia ya maridhiano hivyo , tunaishukuru ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutujengea uwezo mara kwa mara kwa kupewa semina mbalimbali ili kuondokana na Migogoro kwenye vyama vyetu vya siasa “amesema Katibu Mkuu huyo wa Act Wazalendo.

Naye, Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokratic Part (DP) Philipo Fumbo ameishukuru ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kuandaa mafunzo hayo ,huku akibainisha kuwa vyama vingi vya upinzani havina ruzuku kutoka serikalini hali inayochangia kushindwa kuajiri wahasibu na maafisa ununuzi nakupeleekea ubadhilifu wa fedha na matumizi mabaya ya fedha.

Mafunzo ya Siku Mbili Kwa Viongoz wa Vyama vya Siasa yamelenga katika maeneo mbalimbali imkiwemo kujifunza kuandaa Taarifaya fedha ya kuawasilisha kwa CAG,pamoja na kuandaa Matamko ya Mali za Chama hadi kufikia Mwezi Septemba Mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!