Home Kitaifa HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUKAMILISHA VYUMBA VYA MADARASA KABLA YA JANUARI

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUKAMILISHA VYUMBA VYA MADARASA KABLA YA JANUARI

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

Serikali imetoa shilingi Million 580 kwaajili ya ujenzi Madarasa 29 ya Sekondari katika kata zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Tanga ambapo yanatakiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na hatimaye kuanza kutumika kwa muhula mpya wa masomo wa mwaka 2023.

Mara baada ya kutoa fedha hizo serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini zilizopokea fedha kwaajili ya miradi hiyo kukamilika December 31, 2022 ambapo katika kuhakikisha mkoa wa Tanga unaendana na maagizo hayo mkuu wa mkoa Omari Mgumba aliagiza Madara yote yanayotekelezwa na fedha hizo yakamilike na kukabidhiwa November 15 mwaka huu.

Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana amesema kuwa katika kuhakikisha wanatekeleza maagizo hayo na kutimiza adhima ya serikali tayari mchakato wa ujenzi wa miradi hiyo umeshaanza kwa hatua ya za awali ikiwemo uchimbaji wa msingi kwa baadhi ya maeneo.

Tuna miradi ya maendeleo ambayo Mheshimiwa Rais ametoa fedha kwakweli hatuna budi kumshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi mia tano themanini kwaajili ya ujenzi wa madarasa 29 yaliyopo ndani ya jiji la Tanga”

Sasa hivi ndio tumeanza utaratibu wa ujenzi wa madarasa na tayari baadhi ya madarasa misingi imeshaanza kuchimbwa na mengine tumeshaanza utaratibu wa kuwapata mafundi, matofali yameshaanza kusambazwa katika shule zote zinazojengwa kwenye shule za Sekondari za Kiomoni, Ummy Mwalimu, Tanga ufundi, Hoten, Kirare, Marungu pamoja na Chongoleani na sasa hivi tunachoendelea nacho kote huko ni kupelekea vifaa vyote ili ujenzi uweze kuanza mara moja” alisema Dkt. Liana.

Tumeweka timu za kusimamia hayo madarasa tunanunua taa za kumulika ili kuhakikisha usiku na mchana ujenzi unafanyika na tutahakikisha hatumuangushi Rais katika ujenzi huu” aliongeza.

Aidha Dkt Liana ameongeza kuwa wanaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani kwa wakina mama, vijana na watu wenye ulemavu ambapo katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/2023 wametoa zaidi ya shilingi Million 300 kwa vikundi vya wajasiliamali.

Alisema katika kuhakikisha mikopo hiyo inawanufaisha walengwa halmashauri hiyo imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwa vikundi vinavyopata mikopo hiyo namna jinsi ya kuitumia vyema ili iwaletee maendeleo na hatimaye kufanya marejesho kwa wakati.

Tuna utaratibu pia wa kuhamasisha vijana wakina mama na watu wenye ulemavu waweze kuja kuomba mikopo, wataalamu wetu tumewapanga waweze kuwasaidia kupata mikopo hii isiyo na riba tunahimiza wananchi wa Tanga waje tutawapa mafunzo na kuwaelekeza namna ya kuomba hasa vijana tuna programu nyingi Sana tumeziandaa kwaajili yao, ili vijana wasitumike kwenda kwenye makundi ya kiuhalifu” alisema Liana

Akiwa katika kikao Cha baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 mstahiki meya wa jiji la Tanga Abdurahman Shillow amewataka Madiwani watendaji pamoja na viongozi wote katika kata zote zinazotekeleza miradi hiyo ya shule kuhakikisha wanashirikiana kuisimamia kwenye ujenzi iuweze kuendana na kasi ili kukamilika kwa wakati.

Sasa hivi tuna miradi ya madarasa 29 ambayo tumepata fedha kutoka kwa Rais kwaajili ya kuepuka uhaba wa madarasa kwenye mwaka wa masomo wa 2023 niwaombe sana kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kama tulivyoelekezwa haya yatafanikiwa ikiwa sisi Madiwani tutatoa ushirikiano wa kutosha lakini mahali popote kwenye changamoto basi sisi tuanze kuzitatua kule kwenye kata zetu” alisema Shillow

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!