Home Kitaifa DEREVA WA DALADALA MBARONI TUHUMA ZA KUMUUA MPENZI WAKE

DEREVA WA DALADALA MBARONI TUHUMA ZA KUMUUA MPENZI WAKE

Na Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamataMaarifa Hadith Matala (45), Dereva wa daladala, mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungokwa tuhuma za mauaji yampenzi wake, Sharifa Twaha Nyamaishwa(31), Kondakta wa Daladala aliyekuwa mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili na kumuua, tukio hilolimetokea tarehe 16 Agosti 2022 huko maeneo yaKimara Suka, na mara baada ya tukio hilo mtuhumiwaalitoweka.

Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo lilianza upelelezi na ufuatiliaji wa haraka na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mkoani Lindialipokuwa amejificha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa wapenzi hao walikuwa na migogoro inayosababishwa na wivu wa kimapenzi na kupelekea kugombana mara kwa mara,namwili wa marehemu ulikutwa na majeraha.

Uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya tuhuma hizo za kikatili uliovuka kiwango.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limemkamata Gamariel Swai (43) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi kwa tuhuma za kuuza spea za magari zilizoibwa kwenye magariya watu mbalimbali .Duka lake lipo Mtaa wa Songea, Ilala.

Awali Jeshi la Polisi tarehe 23 Julai 2022lilipokea taarifa ya wizi wa vifaa vya gari huko maeneo ya Kivule bombambili Ukonga ambapo Sifael Msemwa (38) mkazi wa Bombambili aliibiwa vifaa vya gari yake aliyokuwa ameiegesha nyumbani kwake aina ya Toyota Prado yenye usajili namba. T.429BKK ambavyo ni side mirror 03,power window 04, control box na betri la gari.

Tarehe 15 Agosti 2022 baada yaupelelezi alikamatwa mtuhumiwa Gama Swai na katika upekuzi katika duka lake Namba 21 lililopo mtaa wa Songea, Ilala alikutwa na side mirror 02 na power window 04 zilizoibwa toka katika gari hilo Toyota Prado.

Aidha vilikamatwa vifaa vingine mbalimbali vya magari dukani hapo vinavyodhaniwa kuwa nivya wizi kutokana na kutokuwepo namaelezo ya kutosha kuhusiana na vifaa hivyo. Vitu vilivyokamatwa ni .

Taa za mbele 93 za magari ya aina mbalimbali, taa za nyuma 130 za magari ya aina mbalimbali,power window 189 za magari ya aina mbalimbali,side mirror 62 za magari ya aina mbalimbali, show za mbele za magari 07 mbalimbali, show za ndani za magari 35 za aina mbalimbali, mikono ya milango (vitasa) 26 za magari, rejeta 01na betri moja.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparasheni kali dhidi ya watu wanajihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja wizi wa magari na uuzaji wa vifaa vya magari vitokanavyo na magari ya wizi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!