
Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Kwimba ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi inazochukua katika ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.
Ngw’ilabuzu alisema hayo Jana 3/2/2025 katika eneo la Wilaya ya kwimba katika mwendelezo wa ziara za kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani hapo.
Wakiwa katika Ziala ya kamati ya Siasa walitembelea Shule ya Sekondari ya Dk Samia iliyopo katika Kata ya Malya iliyojengwa kwa zaidi ya milioni 500 kutokana na fedha za serikali kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Thereza Lusangija alisema, Ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, jengo moja la utawala, Maabara ya Kemia, Fizikia na Biolojia.
Aliongeza kusema kuwa vilevile imejengwa Maktaba, chumba cha kujifunzia Masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), matundu 11 ya choo na kichomea taka.
Ludigija,alisema manufaa ya mradi huo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi, kupunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu, utoro, mimba za utotoni