Home Kitaifa CHANDI AWATAKA WANACCM MUSOMA MJINI KUWA MARAFIKI NA KUACHA MAKUNDI

CHANDI AWATAKA WANACCM MUSOMA MJINI KUWA MARAFIKI NA KUACHA MAKUNDI

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Patrick Chandi amewataka wanachama wa chama hicho kuwa marafiki na kuepuka makundi.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Musoma mjini kwenye ukumbi wa CCM mkoa.

Mwenyekiti huyo wa mkoa amesema katika uongozi wake hapendi kuona watu wakitofautiana hususani makundi ambayo hayakijengi chama.

Amesema watu wanapokuwa marafiki hawawezi kuwa na majungu na kuwataka kuwa wamoja wakati wote.

Chandi amesema wanachama wanapaswa kukisemea vizuri chama kwa kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi za miradi katika sekta mbalimbali.

Amesema licha ya kuisemea serikali ni muhimu kuwa na vikao vya chama kuanzia ngazi ya matawi ili kufanya uimalishaji wa chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma mjini Benedict Magiri amesema ili chama kiendelee kusjika hatamu ni vyema baadhi ya wanachama kuacha kuwachonganisha viongozi.

Amesema wapo wanaokwenda kwa viongozi kwa kufikisha mahitaji yao lakini kabla ya kueleza ya kwao wanatoa maneno ya kuchonganisha.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amemueleza Mwenyekiti wa mkoa kuwa ndani ya jimbo ilani imetekelezwa kwa asilimia 100.

Amesema sekta za elimu,afya,maji na miundombinu iko vizuri kwa kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha za kutosha katika kutekeleza miradi hiyo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara yupo kwenye ziara ya wilaya zote za mkoa kufatilia utekelezaji wa ilani na kusikiliza kero za wananchi.

Previous articleMKUU WA WILAYA YA SAME KASILDA MGENI AMEWATAKIA MTIHANI MWEMA KIDATO CHA NNE
Next articleJELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABISHIA UJAUZITO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here