

Wamiliki wa Migodi ya Uchimbaji Madini nchini wametakiwa kuzingatia masharti ya Leseni za Uchimbaji Madini pamoja na kulipa fidia kwa wakati.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Madini Msafiri Mbibo Oktoba 10 ,2023 alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida.
Akiwa katika Mgodi wa Shanta Naibu Katibu Mkuu Mbibo ,aliutaka mgodi huo kuzingatia taratibu za Ushirikishwaji Jamii sehemu za Migodi (Local Content) pamoja na Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kama vile kurudishaji faida kwa jamii inayozunguka mgodi
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu , ametembelea Mgodi wa Shanta wa Uchimbaji Madini ya Dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mine.
Ziara hiyo ya kikazi yenye lengo la kujionea maendeleo ya sekta ya Madini mkoani Singida Naibu Katibu Mkuu aliambatana wataalam kutoka Wizara ya Madini.


            







