Home Kitaifa MCHANGO WA MBUNGE MUHONGO WA SHUGHULI ZA MWENGE WAPOKELEWA

MCHANGO WA MBUNGE MUHONGO WA SHUGHULI ZA MWENGE WAPOKELEWA

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma vijijini Denis Ekwabi amepokea na kuwasilisha mchango wa mbunge Prof.Sospeter Muhongo kufanikisha shughuli za mwenge.

Akiwasilisha mchango huo kwaajili ya huduma za chakula kwa viongozi wa Kata ya Kiriba amesema mchango huo ni muhimu katika kufanikisha shughuli hiyo.

Amesema Muhongo amekuwa mchangiaji mkubwa katika masuala mbalimbali katika jimbo la Musoma vijijini.

Ekwabi amesema mchango uliotolewa na mbunge huyo ni pamoja na Ng’ombe,mchele,mafuta,maji ya kunywa pamoja na viungo vyoye vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2,416,000.

“Tunamshukuru sana mheshimiwa Muhongo kwa mchango wake katika kufanikisha shughuli za mwenge kwenye eneo letu”

Mbunge yupo kwenye shughuli za bunge Dar es salam lakini tumepokea mchango wake kwaajili ya kufanikisha hasa katika eneo la chakula” amesema Ekwabi.

Amesema viongozi na wadau wengine wanapaswa kujitoa na kuchangia kwaajili ya kufanikisha masuala mbalimbali.

Wakipokea mchango huo viongozi wa Kata ya Kiriba utakapofanyika mkesha wa mwenge wamemshukuru mbunge huyo kwa mchango alioutoa.

Wamesema watu wanaojitoa kwaajili ya kuchangia jambo lifanikiwe sio wote kama ambavyo amekuwa akifanya mbunge huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!