Home Kitaifa WASHINDI WA TATHMINI YA UBORA WA HUDUMA HOSPITAL YA RUFAA MARA WAPEWA...

WASHINDI WA TATHMINI YA UBORA WA HUDUMA HOSPITAL YA RUFAA MARA WAPEWA ZAWADI

Na Shomari Binda-Musoma

IDARA ya ubora wa huduma hospitali ya rufaa mkoa wa Mara imetoa zawadi kwa washindi wa tathmini ya ubora wa huduma ambapo washindi wamepatikana baada ya kushindanishwa kwa idara zote zinazopatikana hospitalini hapo.

Akiwataja washindi hao, Mwenyekiti wa idara ya ubora wa huduma,Venance Bwire, amesema idara ya upasuaji imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na idara ya ICU huku CTC ikishika nafasi ya tatu.

Akuzungumza mara baada ya washindi kukabidhiwa zawadi,Mwenyekiti hiyo amesema utaratibu huo unaofanywa na hospital unaongeza chachu ya ufanyaji kazi.

Amesema idara zote hospitalini hapo zinafanya kazi nzuri ambapo katika kipindi cha miezi mitatu hakuna malalamiko ambayo wameyapokea kutoka kwa wanaopatiwa huduma.

Bwire amesema zoezi hilo ni endelevu kuwa linafanywa katika kila kipindi cha miezi mitatu ili kuangalia tathimini ya utoaji huduma.

Huduma kwenye hospital yetu ya rufaa ya mkoa wa Mara ni nzuri hutujapata malalamiko kwa kipindi hiki na tunaendelea kuboresha utoaji huduma”, amesema Bwire.

Aidha Bwire amesema idara zilizopiga hatua katika viwango vya ubora kuwa ni utawala pamoja na wodi ya wazazi (Post Natal Ward) ambao pia wamejinyakulia zawadi sanjari na vyeti.

Mashindano haya hufanyika kila baada ya miezi mitatu ambapo idara zote hushindanishwa katika viwango vya ubora wa huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!